Mama Makinda hataki Uspika.. mengine matatu>> miaka 40 Bungeni, kelele? wanaogombea?


Tayari wanachama 21 wamejitokeza kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuliongoza Bunge la 11 litakaloanza siku chache zijazo.
Kuna Magazeti ambayo yaliandika stori na kumtaja Spika wa Bunge aliyemaliza muda wake, Mama Anne Semamba Makinda kwamba na yeye yumo kwenye list ya wanaogombea nafasi hiyo… November 13 2015 ametoa majibu juu ya msimamo wake >>> ‘Nimetumikia Uspika kwa miaka mitano kihalali, nimeona nisiendelee kugombea Uspika… Maisha yangu yote nimetumikia Siasa, nimeingia Bungeni wengine mlikuwa hamjazaliwa, mpaka October 2015 nimetimiza miaka 40.’- safari yake kwenye Siasa ilianza hivyo.
makinda
Kwa nini hautaki tena Uspika? >>>’Sioni kama nina sababu ya msingi ya kuendelea kugombea kwa miaka mingine mitano, ukiangalia wa rika yangu wote wamestaafu, mheshimiwa Kikwete ni rika yangu amestaafu, wote niliosoma nao wamestaafu, naona ni vizuri tukawaachia wengine, si kwamba hatutakuwa na ushirikiano nao, tutatoa ushirikiano kwa kiongozi yeyote atakayetaka‘>> Mama Anna Makinda.
Kwenye sentensi nyingine Mama Anne Makinda ana haya kuhusu safari yake ndani ya Bunge >>> ‘Mimi maisha yangu yote nimelitumikia Bunge, nimekuwa Waziri wa shughuli za Bunge, nimekuwa Mwenyekiti, Naibu Spika na hata Spika, nimekwenda ngazi kwa ngazi…sasa ukifika miaka 40 ni vizuri ukaona wengine nao wanataka kufanya nini‘ >>>> Mama Makinda.
Uliona vurugu zozote Bungeni? Majibu ya mama Makinda kuhusu zile purukushani ni haya hapa >>> ‘Nilienjoy sana Bunge kwa sababu mimi mwenyewe asili yangu ni fujo kidogo, rafiki zangu wale ninawamisi sana‘- Mama Makinda.

Maoni