MANENO YA KIKWETE BAADA YA KUSTAAFU



Ikiwa leo Novemba 5, 2015 ndio Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amemaliza muda wake wa kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku Dk.John Pombe Magufuli akiapishwa kama rais wa awamo wa 5 wa kuliongoza taifa hili.Sasa kupitia kwenye akaunti ya twitter ya Jakaya Mrisho Kikwete ameyaandika haya maneno kuhusu kulitumika taifa la Tanzania kwa miaka 10..’Miaka 10 imekwisha. Imekuwa safari nzuri na yenye mafanikio makubwa kwa nchi yetu. Taifa letu litabaki salama. Nawatakia kila la kheri’ – Kikwete

Maoni