Fisi wa ajabu
Kiteto.Watoto wawili wa
familia moja Kijiji cha Kijungu wilayani Kiteto mkoani manyara, wamenusurika
kifo kwa kuokolewa na mbwa wao baada ya fisi kutaka kuwaua wakati wakichunga
mifugo yao.
Ofisa mtendaji wa Kijiji cha
Kijungu Bw.Jula Jula amewataja watoto hao kuwa ni Danniel Gabriel (8) na
Olowassa Christopher (12) wa Kijiji cha Kijungu kuwa fisi hao wamekuwa tishio
katika maeneo yao
Alisema watoto hao waliona
fisi wakiingia ndani ya shimo kisha
kusogelea na ndipo wakatoka na kuanza kuwashambulia na kutaka kuwaingiza ndani
ya pango hilo
Wakati fisi wakikamata watoto
hao mbwa wao alikuwa akibweka kwa kuona watoto hao wanazamishwa ndani ya shimo
ndipo fisi akang’atwa na kushindwa kumwingiza mtoto ndani ya shimo na kuanza
kushambuliana na mbwa kisha watoto kutoroka
Kutoroka kwa watoto hao kuliacha
kibarua kigumu kwa mbwa wao ambaye muda mfupi aliuawa kisha kuingizwa kwenye
shimo lao ambalo hulitumia kama makazi ya kila
siku
Ofisa huyo wa Serikali
alisema watoto hao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kilindi kwa matibabu
zaidi na kwamba hali zao bado hazijaimarika kutokana na mjeraha waliyopata
kwenye mkasa huo
“Watoto hawa wamekimbizwa hospitali
ya Kilindi ambako ni karibu tofauti na Kiteto ambako ni mbali kwa lengo la
kuokoa maisha yao
kutokana na majeraha waliyoyapata”alisema Jula
Kwa upande wa baadhi ya
wananchi wakizungumza na MWANANCHI walisema fisi hao wamezoea kuleta madhara
katika maeneo hayo na kuiomba Serikali kuingilia kati kuzuia madhara zaidi
Kamanda wa Polisi Christopher
Fuime amethibitisha tukio hilo
huku idara ya maliasili ikitakiwa kufika katika maeneo hayo kuona namna ya
kuwasaidia wananchi hao juu ya wanyama hao
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni