Nabii TB Joshua. |
Kutoka kwenye Moja ya account za
mitandao ya kijamii zinazoendeshwa na huduma ya T.B Joshua zimewekwa
Picha zinazomuonesha nabii Temitope Balogun Joshua au maarufu kama T.B.
Joshua ambaye alizaliwa June 12, 1963 nchini Nigeria na amekua kiongozi
wa kanisa kubwa nchini Nigeria lijulikanalo kama The Synagogue, Church
of All Nations (SCOAN) ambapo kanisa hilo pia linaendesha kituo cha
televisheni chan Emmannuel TV.
Mtumishi huyu wa MUNGU amehusika katika
miujiza mingi na maelfu ya watu wamefunguliwa na kupokea uponyaji
kutokana na huduma ya Nabii TB Joshua.
Moja ya Shule alikosomea TB Joshua. |
Nabii T.B Joshua ametokea kujitwalia umaarufu sana katika
nchi nyingi za Afrika na barani Ulaya na Asia kwa kutabiri mambo
mbalimbali ambayo baadae yalikua yakitokea kweli na kuripotiwa na vyombo
mbalimbali vikubwa na vinavyoheshimika Duniani.
Nyumbani kwako Tb Joshua, mahali alipozaliwa na kukulia. |
Nabii T.B Joshua alipokua na umri wa miaka 25 |
Nabii T.B. Joshua pia amewahi kutambulika kama moja ya
watu 50 toka Afrika wenye nguvu ya Ushawishi kwa jamii wadhifa aliopewa
na taasis ya Pan-African magazines na pia kumtaja kama moja ya watu
maarufu sana Duniani
Nabii T.B Joshua alipokua na umri wa miaka 20 |
Nabii T.B Joshua alipokua na umri wa miaka 17 |
Moja ya mikutano ya injili ya TB Joshua huko Mexico |
Maoni
Chapisha Maoni