MUHIMBILI WAPEWA SIKU TATU ZA MKUJIREKEBISHA


Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue jana alifanya ziara katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikiwa ni muendelezo baada ya Rais Dk. MAGUFULI kufanya ziara ya kushtukiza.

Baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukagua vitanda vilivyonunuliwa baada ya agizo lake, Sefue alitoa maamuzi yaliyofikiwa…
 
Majibu kutoka Ikulu kuhusu mashine za CT Scan na MRINimekagua mashine hizi za kukagua magonjwa MRI na CT Scan, chanzo cha kuharibika tena ni kukaa muda mrefu bila kutumika,sasa hivi spea zote zimefika, kazi ya kutengeneza inaendelea, MRI nimehakikishiwa ndani ya siku tatu itakuwa inafanya kazi, kuhusu CT Scan nimeambia kesho(leo) inaweza kuanza kufanya kazi”..
 
“Lazima mafundi kutoka Philips  wakae muda wa wiki moja baada ya kutengenezwa kujiridhisha zimekamilika..bado tuna mpango wa kuongeza mashine hizi ili angalau tume na mbili mbili..,kuhusu madeni ya mshine hizo..
 
"Ni kweli kulikuwa na madeni lakini tumeanza kuyalipa kwa sasa suala hilo halipo tena, tulikuwa tunadaiwa na Philips bilioni 7 na Serikali tayari ililipa bilioni 3 nyingine zinapaswa kulipwa na waliokuwa wakipata huduma ya mashine hizo“… Ombeni Sefue.

Maduka ya Bohari ya dawa MSD kujengwa ndani ya hospitali kubwa..“Tuna tatizo la kibajeti, tunahitaji bajeti ya kama bilioni 248, bajeti unakuta inafikia kama bilioni 70, hili inabidi tushughulike nazo hasa katika hospitali kubwa pamoja na zile za rufaa, MSD wanapaswa kufungua maduka yao ndani ya hospitali..na lazima kuwa na dawa zote, hospitali ya Muhimbili duka la madawa litafunguliwa rasmi Jumatatu”..Ombeni Sefue.
 
Ishu ya wizi wa dawa za Serikali pia imesikika...“Tutumie mifumo ya TEHAMA kuhakikisha hakuna dawa ya Serikali inaibiwa, pia tujue kwamba kila dawa inatumiwaje na daktari, ufumbuzi wa matatizo haya upo, kwa wale wa maduka ya dawa binafasi ambao wanajijua wanatumia dawa za serikali michezo hiyo, basi, dawa zetu tutakuwa tunaziwekea nembo, ukigundulika ujue mwisho wako basi, mnapaswa kutambua dawa hizi zinanunuliwa na kodi ya wananchi hivyo tutadhibiti tabia hii” ...Ombeni Sefue.
 
Huduma mbaya kwa wagonjwa “Tutoe huduma nzuri kwa wananchi, tuwahudumie kwa upendo na wakati,  kuanzia sasa kila mtumishi wa umma lazima avae jina lake ili anayemuhdumia ajue anahudumiwa na nani, nitaanza na mimi..ili ikitokea malalamiko ajue anaanzia wapi, na lazima kila ofisi iwe na dawati la msaada ili kila mwananchi aweze kupiga simu na kuweza kutatuliwa tatizo lake”Ombeni Sefue.
 
Kuhusu safari za nje kwa viongozi...“Tumetumia fedha nyingi sana kwenda nje, nyingine za lazima na nyingine sio za lazima, mfano mafunzo sasa ni mwisho, tunavyo vyuo vingi vyenye uwezo wa kutoa mafunzo badala ya kwenda nje ama ni rahisi kuleta mtaalam hapa kuliko kupeleka watu 10 kwenda kwenye mafunzo..
 
"Sasa hivi itakua mbinde mtu kuweza kusafiri..si kwamba hatutahudhuria mikutano lakini Rais amesema mabalozi wetu watatumika pale inapobidi”...Ombeni Sefue.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa Mashine ya CT-Scan katika hospitali hiyo. 23 Novemba, 2015
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (mwenye suti ya kijivu), akimsikiliza mmoja wa Wagonjwa aliyelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), ambayo ilipata vifaa mbalimbali kutokana na agizo la Mhe. Rais la kuboresha huduma katika Taasisi hiyo. 23 Novemba, 2015
Pichani; Mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI) iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambayo inafanyiwa matengenezo. 23 Novemba, 2015
 Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue (wa tatu kulia), akitoa maelezo kuhusiana na ziara yake hiyo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari. 23 Novemba, 2015

Maoni