NA. MOHAMED HAMADA
Mvua kubwa iliyonyesha maeneo
mbalimbali Wilayani Kiteto mkoani
Manyara imesababisha madhara makubwa yakiwemo mtoto mmoja kata ya matui eneo la
kazi ngumu mwenye umri kati ya miaka 10-12 kupoteza maisha na mwingine kijiji
cha Laiseri kuokotwa akiwa hai baada ya kupotea kutokana na mvua hiyo
Katika tukio hilo la mvua pia zaidi ya mbuzi 30 na ngombe
7 zilisombwa na maji kutokana na mvua hiyo na kufa hali iliyosababisha taharuki
kubwa kwa wakazi wa Kibaya na Wilaya ya Kiteto kwa ujumla
Kufuatia hali hiyo Wananchi
wilayani Kiteto wameitaka Serikali wilayani humo kuona namna ya kuwasaidia juu
ya matukio hayo ambayo wengi wao wamepoteza mali
zao kutokana na mvua hiyo na kusababisha kukosa makazi na hata mali zao
Mkuu wa Wilaya ambaye ni
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Samuel Nzoka amekiri kunyesha mvua
hiyo akisema jitihada za Serikali zinaendelea kuona namna ya kutoa msaada kwa
wahanga hao
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni