WAKATI
Maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani yakiendelea kushika
kasi mkoani Singida ambako yalipangwa kufanyika kitaifa mwaka huu Rais
Dr John Magufuli ameagiza maadhimisho hayo kusitishwa .
Rais Dr Magufuli ametoa agizo la kusitisha maadhimisho hayo kupitia kwa Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue leo .
Rais
Dr Magufuli ameagiza fedha hizo zitimike kununua dawa za kupunguza
makali ya ya virusi vya Ukimwi ( ARVs)na vitendanishi vya kupimia Ukimwi
.
Taarifa hiyo tayari imefika ofisi ya Mwenyekiti wa tume ya kuthibiti Ukimwi Tanzania Dr Fatuma Mrisho .
Maoni
Chapisha Maoni