Mkuu wa mkoa wa manyara Dr Joel Bendera mwenye suti nyeusi wa pili kutoka kushoto akienda kuangalia kaya maskini katika moja wa familia kijiji cha Kiperesa
Mkuu wa mkoa wa Manyara Dr Joel Bendera akimtaka mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Kiperesa ambaye ni kikongwe kuhaa huku yeye akikataa kwa kumheshimu
Mkuu wa mkoa wa Mkoa
wa Manyara Dr.Joel Nkaya Bendera ameridhishwa kuona kaya maskini zinazosaidia
na Serikali kupitia mradi wa jamii TASAF na kuagiza elimu zaidi itolewe kwa
wananchi
Akizungumza na wananchi wa
Kata ya Kiperesa na Njoro baada ya kutembelea kaya hizo Dr Bendera alisema
amekutana na walengwa ambao amethibitisha kuwa fedha zilizotolewa na Serikali
zimewafikia huku akisisitiza wataalamu kutoa TASAF kuelimisha jamii zaidi
“Sina shaka na mpango huu wa
Serikali ambao awamu hii tumeamua kuzijengea uwezo kaya maskini kwa kuwapa
fedha keshi ili waweze kukabiliana na umaskini wa kipato tofauti na awamu
zilizopita”
Naagiza TASAF endeleeni
kuelimisha wananchi juu ya nani anastahili kupata msaada huu kwani kila mahali
kumekuwepo na manuguniko ambayo wakati mwingine yanahitaji ufafanuzi tu kidogo
Aliwaasa walengwa kutumia
fedha hizo kujikwamua na umaskini kwa kuanzisha vitu vitakavyo wasaidia na
kuwapongeza baadhi ya walengwa wakiwemo Bi.Mwanahamisi Issa, Mwanaidi Ibrahimu
na Sophia Ramadhani kwa kuanzisha ufugaji kwa fedha hizo
Wakimweleza Mkuu huyo wa Mkoa
walengwa hao walisema fedha hizo zinawasaidia kupunguza makali ya maisha kwa kununua
mahitaji yao
mbalimbali yakiwemo mahindi sambamba na kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku na
mbuzi
Akisoma taarifa ya
utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya maskini Philipo Sengela mratibu wa TASAF
wilaya alisema mchakati wa utambuzi wa
kaya maskini ulianza Julay hadi Agosti 2014
Kaya 7551 zilitambuliwa ambapo
kaya 6140 zilihakikiwa na kuandikishwa, huku kaya 1411 zikidaiwa kutopata
msaada huo kutokana na kutokidhi vigezo ambapo zoezi la malipo lilianza Julay
2015 kwa kaya 6125
Kwa mujibu wa taarifa hiyo
walengwa 15 majina yao
hayajajitokeza kwenye orodha ya malipo huku jitihada zikidaiwa kuendelea
kufanyika ili majina hayo yaweze kuonekana kisha kupata haki hiyo ya malipo
Alisema malipo ya awamu mbili
yamefanyika Julay/ Agost ambapo jumla ya tsh 218,940,000.00 zililipwa kwa kaya
lengwa 5684 ambapo tsh 229,368,000.00 ziliidhinishwa huku kiasi cha tsh
10,428,000,00 zikirejeshwa TASAF makao makuu baada ya walengwa 300 kutojitokeza
Malipo ya mwezi Septemba
Oktoba kaya lengwa 6111 kati ya 6125 zililipwa tsh 217,208,000.00 kati ya tsh
217,640,000.00 zilizoidhinishwa tsh 432,000.00 zilirejesjhwa TASAF Taifa baada
ya walengwa 14 kutojitokeza
Akizungumza kwa niaba ya
walengwa hao Yusuph Madi wa Kijiji cha Kiperesa aliipongeza Serikali kwa kuona
umuhimu wa kuzisaidia kaya hizo akisisitiza mpango huo uwe endelevu sambamba na
kuwataka viongozi wa ngazi mbalimbali kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli
kusukuma maendeleo mbele
Maoni
Chapisha Maoni