Jiji la Dar kwa asilimia kubwa viti vya madiwani vimechukuliwa na UKAWA.Kwa maana hiyo ma meya wa manisipaa na Meya wa Jiji lazima watatoka UKAWA kulingana na wingi wao.Isipokuwa lipo swala lazima viongozi wa juu wa UKAWA walisimamie,Nalo ni mchakato wa kumpata meya wa jiji la Dar
Wote tunajuwa yupo Diwani tajiri kuliko madiwani wote Tz kama si africa mashariki.Diwani huyu zipo fununu zilizagaa kuwa amegombea nafasi hiyo kwa nia ya kuwania umeya wa Jiji la Dar
Sasa najiuliza kwa utajiri wake alionao akiamua kuwahonga madiwani wa UKAWA Hata million 50 kila diwani kwa idadi ya wale watakao mwezesha ushindi yupo diwani mwenye ubavu wa kuzikataa?
Wote tunajuwa wagombea udiwani wengi ni watu wa kipato cha chini.Pili diwani huyo tajiri aki spend Hata million 500 kufanikisha adhima yake ni rahisi kuzirejesha kama akifanikiwa.
Maana millions 500 ni kiwanja kimoja tu kwa jiji la DaR tena kisichokuwa katikati ya mji.Huu ushauri nautoa kama UKAWA wataupuuza baadae watalaumiana wenyewe kwa wenyewe na muda utakuwa umepita tayari. Zipo halimashauri haya yalijitokeza 2010 masikubali kurudia makosa tena.
Kumbukeni: Kufanya kosa si kosa,Bali kurudia kosa ndio kosa kubwa.
chanzo JamiiForums
Maoni
Chapisha Maoni