RAMANI YA MKOA WA MANYARA
Katika kile kilichoelezwa kuwa ni kukaba mpaka penalt Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Kiteto mkoani Manyara kimedhamiria kuufuta upinzani baada ya viti vitatu vilivyochukuliwa na CHADEMA kati ya 20 kupingwa mahakamani
Awali kata zilizokuwa zimetangazwa na msimamizi wa Uchaguzi Kiteto Bosco Ndunguru kuongozwa na CHADEMA ni Matui,Makame, na Loolera huku zingine zilizobaki kushikiliwa na CCM ambapo wamesema wanataka kufuta upinzani kwa kuhakikisha CCM inatawala kila kona
Mmoja wa viongozi wa CCM ngazi ya wilaya akizungumza na MWANGANAMATUKIO alisema haoni nguvu ya upinzani Kiteto akisisitiza kilichopo ni chuki inayosambazwa na watu wachjache kukichukia chama akisema safari hii wanaenda kuwatumikia wananchi ipasavyo
Maoni
Chapisha Maoni