Prof. Lipumba: CHADEMA wamepoteza dira

 
 
Wakati akiongea kupitia AzamTwo Television, Prof. Lipumba amesikika akisema, CHADEMA kimepoteza dira ya kisiasa kutokana na mtafaruku uliojitokeza ndani ya UKAWA baada ya kumpokea Lowassa na kumfanya mgombea Urais wa Tanzania.

Prof. Lipumba amesema, ??Sisi ndani ya CUF tunaweza kukijenga vizuri chama chetu kwa sababu msingi wetu ni kusimamia haki kwa wote lakini wenzetu wa CHADEMA wamepoteza dira kwa sababu itakuwa ni vigumu kuzungumzia suala la mapambano dhidi ya ufisadi??.

??Msingi wa sera zetu ni Haki Sawa Kwa Wote, Rais Magufuli anasema HapaKaziTu na sisi tunasema Hapa ni Haki Tu ?? Alisema.

Aliendelea kusema, ??Tuna mahala pazuri pa kuanzia, kutazama namna ya kuikosoa serikali katika kutekeleza hizi sera za HapaKaziTu, Je tunalinda haki za kila mmoja wetu, tunafuata utaratibu mzuri wa sheria??

Alimalizia kwa kusema, ??wenzetu CHADEMA wamepoteza dira??.

Maoni