MOHAMED HAMAD
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Pili Mgogo (28) mkazi wa
Kibaya wilayani Kiteto mkoani Manyara, aliyekuwa amepelekwa hospitali
ya Rufaa Dodoma kutoka Kiteto baada kujilipua kwa mafuta ya petroli
kwa madai ya wivu wa mapenzi amefariki dunia
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni mjini Kibaya eneo la shule ya
Kaloleni, akitaka kujiua kwa rafiki yake huyo wa kiume ambaye siku
hiyo hakuwepo kwa madai ya kupata manyanyaso kutoka kwake yakiwemo
kuona baadhi ya nguo za mwanaume huyo zikiwa zimevaliwa na mwanamke
mwingine
Kutokana na alivyokuwa ameungua tulishindwa hata kumbeba kumpeleka
Hospitali, lakini baadaye tukalazimika kuwajulisha polisi ambao
walikuwa na gari lao kisha kumchukua na kumpeleka hospitali ya kibaya
ambako alitibiwa na baadaye kuhamishiwa Dodoma kwa matibabu
zaidi,alisema mmoja wa mashuhuda
“Nilisikia kishindo cha kuwaka moto ndipo nikataka kujua kulikoni na
ndipo hapo nikaona nisogee kisha kuona mwanamke huyo anavyo waka moto,
nilikimbia na kuleta maji huku wengine wakimwagia mchanga kwa lengo la
kuzima moto huo”
Kwa mujibu wa Daktari aliyekuwa anamtibu wa hospitali ya wilaya ya
Kiteto ambaye hakutaka kutaja majina yake alisema jitihada za kumwokoa
mgonjwa huyo ziliendelea ingawa hali yake haikuwa inaimarika na kuamua
kumhamishia Dodoma kwa maditbabu zaidi
“Majeruhi ameungua maeneo mbalimbali ya mwili wake kwaanzia kichwani
hadi miguuni,jitihada zimefanyika kuokoa maisha yake ingawa hali bado
sio shwari kutokana na moto huo kuwa umemuunguza sana”alisema
madaktari huyo
Kwa upande wake Said Issa shuhuda wa tukio hilo alisema moja ya sababu
ya mwananmke huyo kujiunguza ni wivu wa kimapenzi, kwani mpenzi wake
alimwacha kisha kuona tishert ya mume wake ikiwa imevaliwa na mwanamke
mwingine na kuamua kufanya maamuzi hayo magumu
Wivu wa kimapenzi wilayani Kiteto umeshamiri kwa jinsi zote ambapo
wengi wa wanaume na wanawake wamedaiwa kujinyonga huku wanawake
wakinywa sumu na hata kujiunguza kwa moto kwa lengo la kujiua
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Manyara kamishna msaidizi Christopher
Fuime alithibitisha kutokea tukio hilo akisema upelelezi unaendelea
kujua chanzo halisi cha tukio hilo na wameanza kuhojiana na mashuhuda
wa tukio baada ya kifo hicho
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni