DC Kiteto amwoka mwanafunzi asiolewe



MOHAMED HAMAD
Mkuu wa wilaya ya Kiteto mkoani manyara kanali Samuel Nzoka, amemwokoa
mwanafuzi wa darasa la nne wa miaka (12) wa shule ya msingi Twanga
kata ya Namelock aliyekuwa aozeshwe kwa mwanaume kwa kuanza msako wa
kumkamata Palesoi Kiloriti mzazi wa mtoto huyo

Mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa alitoroka nyumbani kwao
jana, kisha kwenda kwa mmoja wa wanajamii kijijini hapo kuomba msaada
wa kuzuia jitihada za mzazi wake kumwozeshe kwa mwanaume ambaye tayari
ilidaiwa leo hii atawafungisha ndoa

Akizungumza na MTANZANIA mkuu wa wilaya ya Kiteto Kanali Samuel Nzoka
amesema jitihada za kumkamata mzazi huyo zimeanza na kumtaka
ajisalimishe mwenyewe ofisini kwake ili sheria ifuate mkondo wake

“Kwa dunia ya leo huwezi kumwozesha mtoto wa miaka 12 kwa mwanaume ili
hali unajua kuwa anasoma na hata umri wake pia hauruhusu kufanya hivi
sasa nataka ajisalimishe mwenyewe ofisini kwangu sheria ifuate mkondo
wake” alisema kanal Nzoka

Mtoto huyo amehifadhiwa katika moja ya shule zilizopo wilayani Kiteto
ili aweze kuendelea na masomo ambapo taarifa za awali zinaeleza kuwa
imekuwa ni mazoea kwa baadhi ya wanajamii wilayani humo kutumia watoto
wa kike kama vyanzo vya mapato yao na familia

Vitendo vya wazazi kuozesha wanafunzi wa kike wilayani Kiteto
vimekithiri wakilenga kupata mahari kwaajili ya kuendesha maisha yao
ambapo kwa hivi sasa imedaiwa kuwa ni gharama kubwa hasa kwa jamii ya
kifugaji maasai

“Ukitaka kuoa kwa jamii ya kifugaji mwanaume analazimika kutoa ng’ombe
6-8 ambapo mzazi hukabidhiwa kabla ya kuolewa motto wake, huku mali
hiyo ikidaiwa kuwa huwa ndio mali ya familia”alisema kimirey Kaiser wa
jamii ya kifugaji

Kwa upande wake Maulidi Kijongo (mwananchi) alisema tatizo la
wanafunzi kuolewa linasababishwa na wazazi pamoja na viongozi
waliopewa mamlaka na wananchi kusimamia sheria

Alisema baadhi ya waalimu wakuu wamekuwa vinara wa kumaliza kesi hizo
kwa kutotoa taarifa za kweli kuhusu kuozwa kwa watoto hao huku
wakibakia kuandika utoro wakati kulikuwa na uwezekano wa kuzuia kwa
kukataa watoto wasiolewe

“Sijawahi kusikia mtu kafungwa kwa kumwozesha mwanafunzi hapa kibaya
ila kesi za namna hiyo huwa zinakuwepo lakini zinavyoisha huwezi kujua
hatimaye unaona mtu yupo huyu mitaani alisema mmoja wa wananchi

mwisho

Maoni