UHABA WA MAJI KITETO WAGEUKA KUWA KERO



Mmoja wa akina mama akiwa katika harakati za usafi mjini kibaya katika korongo la darajani ambalo hutumiwa na wananchi kuchota maji ya kunywa

Mmoja wa vijana wa mji wa Kibaya akiwa katika hatakati za kusaka maji kwaajili ya kuuza ndoo moja ni sh 500



Maji yanayochotwa eneo la ngarenaro na kutumiwa kwaajili ya shuhuli za kibinadamu korongo la darajani wilayani Kiteto mkoani manyara, hayastajili kutumika kutokana na chanzo hicho kuharibiwa kwa kumwagwa takataka ngumu zinazokusanywa mjini Kibaya

Wataalamu waliobobea katika tafiti wa maji na matumizi yake wamesema chanzo hicho hakistahili kutumika kwa matumizi ya binadamu, kutokana na sababu mbalimbali ambazo zimeelewa ziaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa yakiwemo kipindupidu

Akizungumza na DIRA mmoja wa wananchi wa eneo la ngarenaro anasema pamoja na kutambua kuwa maji hayo si safi na salama kwa afya za watu, wanalazimika kuyatumia ili waweze kuishi…

Hata hivyo wakati kukiwa na tatizo hilo la maji ambalo linatishia uhai wa watu, baadhi ya wananchi wamekuwa wakinufaika na uhaba huo wa maji

Vijana wa Kibaya mjini,wamedaiwa kunufaika na uhaba wa maji kwa kuuza bei kubwa mara wanapoyapata huku uongozi wa mamlaka ya maji wakidai jitihada zinaendelea kutafuta ufumbuzi

Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa manayara Dr Joel Bendera akiwa ziarani Kiteto aliitaka timu ya wataalamu kutoka mkoani kufanya utafiti wa sababu za Kiteto wananchi kutopata maji

Maoni