Mgeni rasmi wa bonanza day Mkuu wa wilaya ya Kiteto Kanal Samuel Nzoka mwenye traki ta blue na mkuu wa polisi Kiteto afande Katabazi wakiwa tayari kiwanjani kuangalia mambo mbalimbali yaliyoandaliwa siku hiyo picha na hisani ya Polisi Kiteto.
Timu ya magereza na polisi wakivutana kamba bonanza day mjini kibaya hivi karibuni mambo yalikuwa murua ona...
Maandalizi ya mtanange mpira wa miguu kati ya timu ya polisi na ya magereza zote za kiteto siku ya bonanza day hivi karibuni...
Mchezo wa kufukuza kuku kama unavyoona hapa..kati ya magereza na polisi zote za kiteto siku ya bonanza day..
Mchezo wa kukimbia na mifuko bonanza day lililoandaliwa na Polisi Kiteto kati ya magereza na Polisi..
NA. MOHAMED HAMAD
Katika kile ambacho mtu anaweza kujivunia kwa watu akaeleweka..ni hizi jitihada zinazofanywa na Jeshi la Polisi Kiteto za kujenga mahusiano mema na raia pamoja na taasisi zingine
Katika kile kilichoelewa kuwa ni jitihada binafsi hapa mkuu wa polisi Kiteto John katabazi anaonyesha uwezo wake kujenga mahusiano hayo kwa kuanzisha michezo mbalimbali ona..
Hii ilikuwa bonanza day iliyofanyika mjini Kibaya kati ya Jeshi la polisi Kibaya na Magereza ambapo pamoja na mambo mengine waliweza kushindana
Hapa walikimbiza kuku,walikimbia wakiwa ndani wa mifuko,kulikuwa na mpira wa miguu hali ilikuwa raha mstarehe natamani ungekuwepo...ila shiriki nasi kwa kuangalia picha karibu..
Baadhi ya wadau wa michezo wakizungumza na mwanganamatukio walitaka mkuu wa polisi afande katabazi asikatishwe tamaa na changamoto zilizopo Kiteto za michezo kutotaminiwa wakisema wengi wanatambua mchango wake
"Yule jamaa ana mengi...Kiteto tukimtumia vizuri tutafaidika hata viongozi wa wilaya ambao wanaonekana kutopenda watamuunga mkono tu.."alisema mdau mmoja wa michezo Kiteto
mwisho
Maoni
Chapisha Maoni