MAMEC yapata uongozi mpya

Mkuu wa wilaya ya Babati, Crispin Meela, akipewa maelezo na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari manyara Mamec kabla ya kuanza uchaguzi picha na Mohamed Hamad

Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Manyara Beni Mwaipaja akieleza mkuu wa wilaya ya Babati Crispin Meela mwenye kofia mikakati ya chama cha waandishi Manyara

Kamati ya utendaji ya chama cha waandishi wa habari Manyara mara baada ya kuchaguliwa kuongoza kwa miaka mitatu ijayo




MAMEC yapata uongozi mpya

NA. MOHAMED HAMAD
WANACHAMA wa chama cha waandishi wa habari mkoani Manyara (MAMEC) wamefanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wao watakaoongoza kwa miaka mitatu

Uchaguzi huo umefanyika mjini Babati ambapo aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Benny Mwaipaja ambaye hakuwa na mpinzani amechaguliwa tena kuongoza katika kipindi kingine cha miaka mitatu

Wengine waliochaguliwa ni makamu mwenyekiti Mary Margwe kwa kupata kura (10) dhidi ya Gerce Msovela aliyepata kura (5), nafasi ya katibu amechaguliwa Joseph Simba kwa kura (9) dhidi ya Theddy Challe (6) na katibu msaidizi alichaguliwa Yusuph Dai kwa kura (15)

Nafasi ya mweka hazina alichaguliwa Bi.Judith Peter ambaye hakuwa na mpinzani kwa kupata kura (15) huku mweka hazina msaidizi Mohamed Hamad naye akiwa hana mpinzani akichaguliwa kwa kupata kura (15)

Msimamizi wa uchaguzi ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Babati Crispin Meela aliwatangaza wajumbe wengine watano wa kamati ya utendaji kuwa ni Beatrice Mosses (11) Teddy Charle(12) Abraham Mlundi (13) Restituta Fissoo (14), Joseph Lyimo (15) ambapo Peter Ringo alikosa nafasi kwa kupata kura 10

Akihutubia waandishi hao msimamizi huyo aliwahakikishia kuwa atatoa ushirikiano kwa wanahabari na kuwaahidi kutoa wito kwa viongozi wa Serikali kutumia vyombo vya habari kuharakisha maendeleo ya wananchi

“Kutowatumia waandishi wa habari ni kukosa kujiamini kwa kiongozi na mwisho wa siku wananchi hawatajua serikali imefanya nini na kuwafanya waje kukiadhibu chama kinachosimamia Serikali iliyopo madarakani”alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti mteule wa chama hicho Benny Mwaipaja alimhakikishia mkuu huyo wa wilaya kuwa chama kitakuwa mstari wa mbele kusaidiana na uongozi wa Serikali kueleza mafanikio na changamoto zinazowakabili wananchi

Mwisho





Maoni