Adha ya maji Kiteto, yaifisha maendeleo







NA. MOHAMED HAMAD
WILAYA ya Kiteto mkoani Manyara, inakabiliwa na upungungufu wa maji
safi na salama kwa 64%, hali inayofanya wananchi kutumia muda mwingi
kusaka maji kuliko kufanya shuhuli zingine za maendeleo

Pamoja na jitihada za Serikali na wahisani kuchangia sekta hiyo wilaya
imefanikiwa kuwapa wananchi wake maji safi na salama silimia 36%, huku
kiasi kingine kikidaiwa kupatikana katika maeneo mengine

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Zambia kata ya Lengatei mhandisi
wa maji wilayani humo, Eng. James Kionaumela alisema, hali hiyo
imesababishwa na kukosekana kwa vyanzo vingine vya maji dhidi ya
kutegemea  maji ya kuchimbwa ardhi

“Wilaya ya Kiteto haina mito kama ilivyo katika baadhi ya maeneo
mengine, ili kupata maji safi na salama tunalazimika kuchimba chini ya
ardhi kupata maji, hali inayofanya yapatikane kwa 36%”

Katika kukabiliana na tatizo hilo, wilaya imejenga mahusiano mema na
mashirika yasiyo ya kiserikali, ili kusaidiana kutatua kero hiyo
ambayo imedaiwa kuwachelewesha wananchi kufikia maendeleo tarajiwa

Eng.Kionaumela alisema, kukabidhiwa mradi wa visima viwili vya maji
chini ya shirika la Elewa Africa Association kutoka Switzerland,
kutapunguza makali ya maisha ya wananchi hao, ambayo kila mara
wamekuwa wakitaabika kwa kuchota maji ambayo sio safi na salama
korongoni

“Wananchi mtambue kuwa Serikali imekuwa na mahusiano mema na nchi
wahisani katika kuwahudumia, leo matunda yake ni haya mnayoona, kazi
hii ilipaswa kufanywa na Serikali, lakini leo kwa ushirikiano na
wenzetu mmefanikiwa kupata huduma”

Akiwasilisha taarifa mbele ya Eng. Jemes Kionaumela, mratibu wa Elewa
wilayani Kiteto Fadhili magogwa alisema, shirika limetekeleza miradi
miwili ya maji kijijini hapo ya thamani ya Tsh.84,309,300,50

Alisema miradi hiyo, itanufaisha jumla ya watu 6899 na mifugo 6000, na
kuwaondolea adha ya maji kwa 54%, pamoja na vijiji vya jirani, ambapo
awali walitumia muda mwingi kusaka maji kuliko kufanya shuhuli zingine
za kujiletea maendeleo

Kwa upande wa  Catherine Leboye (mwananchi) Mohamed Bakari Omari
mwenyekiti wa kijiji cha Zambia na Mtendaji wa kata ya Lengatei Kuni
Willson walisema, wananchi walilazimika kutumia masaa nane mpaka kumi
kusaka maji kwaajili ya matumizi ya nyumbani

Mwisho

Maoni