Wananchi:watumishi kuweni wazalendo

                     Mwenyekiti wa halamshauri ya wilaya ya kiteto Lairumbe Mollel akifafanua jambo


Na Mohamed Shabani
WANANCHI wilayani Kiteto mkoani Manyara, wamewataka watumishi kuwa
wazalendo katika utendaji wao wa kazi, ili kuongeza ufanisi wa kazi
utakaoleta tija ambayo itasukuma maendeleo yao mbele

Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi kwa nyakati tofauti, kutokana na
baadhi ya watumishi wilayani humo, kuonekana kukata taamaa, kutokana
na kasi ya Serikali ya awamu ya tano ambayo ina kauli mbiu ya hapa
kazi tu

“Wengi wa watumishi hapa Kiteto wanaonekana kukata tamaa, na hii
imetokana na Serikali iliyopo madarakani ya Rais  John Magufuli,
kuwakatisha tamaa kwa kutowajibika kwai na kubaki kulalamika huku
wasijue wa kuwasaidia”alisema Bakari Maunganya (mwananchi)

Ukifuatilia miradi ya maji, barabara, elimu, na afya yote
inalalamikiwa na wananchi huku viongozi hao wakiendelea kushikilia
nafasi hizo bila kuonyesha japo jitihada za kutafuta ufumbuzi wa
matatizo

Alisema suala la maji wilayani Kiteto, limekuwa sugu kila kijiji
ambapo kauli za viongozi wamekuwa wakisema tatizo liko kwenye bajeti,
Serikali kushindwa kuleta fedha za utekelezaji wa miradi kwa wakati

“Unaweza ukawa na bajeti ya mwaka mzima yenye figa flani, mpaka mwaka
unakamilika, hata nusu ya fedha mliyoomba hamjaipokea, suala hili
limekuwa tatizo sana Kiteto kwa miradi kudorora”alisema Kassimu Msonde
Diwani wa Kata ya Kibaya (CCM)

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Kiteto Bosco
Ndunguru, alisema njia pekee ya kukabiliana na tatizo hilo ni kuongeza
vyanzo vipya vya mapato ya Halamshauri

“Lazima madiwani tubuni vyanzo vipya vya mapato ya Halmashauri, ili
tuweze kukabiliana na tatizo hili, la sivyo kila mwaka tutaendelea
kulia, bila kupata ufumbuzi ambao nauona mimi ni kuongeza
vyanzo”alisema Ndunguru

Mwisho
haban Manyara

Maoni