CELG wabaini ukatili Kiteto

Mohamed Shaban




 Mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi njoro Wilayani Kiteto akiwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara Tanzania akilalamikia ukatili wa kijinsia unaoendelea wilayani humo
 Wasaidizi wa kisheria 25 Wilayani Kiteto chini ya CELG wakiwea katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya mafunzo mjini Kibaya Kiteto Manyara

KITUO cha sheria za mazingira na utawala (CELG), kutoka Dar es Salamu,
kimebaini ukatili wa kijinsia wilayani Kiteto mkoani manyara, hali
iliyofanya kuanzishwa wasaidizi wa kisheria.

Akizungumza na wasaidizi 20 wa kisheria wilayani Kiteto, mwanasheria
wa kituo hicho Elizabeth Maganga alitaja aina za ukatili wilayani humo
kuwa ni ukatili wa kiuchumu, kisaikolojia, kimwili, kingono, ukatili
wa majumbani na mila kandamizi zilizopitwa na wakati

Alisema ukatili huo umeleta madhara makubwa kwa jamii, hali
inayosababisha baadhi ya wananchi kupoteza maisha na wengine kupata
madhara ya kudumu

Alisema hali hiyo imesukuma kituo cha CELG kuamua kuwajengea uwezo
wasaidizi hao wa kisheria ili waweze kuisaidia jamii katika,mapambano
dhidi ya ukatili huo

Akiongea na MTANZANIA Hassan Konki msaidizi wa kisheria Kiteto
alisema, mafunzo waliyopewa na kituo cha CELG yamekuwa na msaada
mkubwa kwao katika mapambano hayo

Kwa upande wake Juma Nyeresa katibu wa wasaidizi wa kisheria Kiteto
alisema idadi kubwa ya kesi za ukatili zimeongezeka na baadhi yao
wameanza kupata haki zao

"Kwa mwezi tunapokea kesi zisizopunga 100 hapa Kiteto na tunachofanya
ni kutoa msaada wa kisheria kwa wahisika kama tulivyopata mafunzo

Akizungumzia ukatili huo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kiteto
Tamimu Kambona alikiri kuwepo alisema elimu hiyo ni muhimu kwa jamii

Alisema ukatili huo ni mkubwa hasa katika maeneo ya vijijini,
wanafunzi kukatushwa masomo kwa kupata ujauzito ama ajira za utotoni
alisema Serikali inaendelea na jitihada za kutaka wananchi kupata
elimu

Mwisho

Maoni