CELG waibua ukatili Kiteto


 Bi Jacklin Barongo wa ustawi wa jamii Kiteto Manyara, akijaribu kuvunja mlango baada ya kubaini kuwepo mtoto akilia ndani kwa zaidi ya masaa matano, aliyetelekezwa na mama yake mzazi mjini Kibaya..
 
Bi. Jackline Barongo kutoka ustawi wa jamii Kiteto akimsaidia mtoto aliyetelekezwa kwa zaidi ya masaa matano ndani baada ya kuvunjwa mlango kufuatilia kelele ya kulia mtoto huyo zilizosikikiwa na majirani mjini Kibaya hivi karibuni wakishirikiana na wasaidizi wa kisheria wa CELG 


Msaidizi wa kisheriia Bi. Rukia akiwa na mtoto aliyetelekezwa ndani kwa zaidi ya masaa matano muda mfupi baada ya kuvunjwa mlango na kuingia ndani kumchukua

 Mtoto aliyefanyiwa ukatili na mama yake wa kufungiwa ndani kila siku kwa zaidi ya masaa matano, hadi mama yake arudi aliyekuwa anafanya kazi ya mgahawani mjini Kibaya Wilayani Kiteto mkoani Manyara Tanzania, ukatili ambao uliibuliwa na wasaidizi wa kisheria wa CELG wakishirikiana na Polisi Kiteto.

Mwanasheria Elizabeth Maganga wa kituo cha utawala wa sheria na mazingira CELG akikabidhi wasaidizi wa kisheria nyaraka mbalimbali vikiwemo vitabu Wilayani Kiteto Mkoani Manyara Tanzania kwaajili ya kufanyia kazi za kisheria .
                                                      xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Kituo cha Sheria za mazingira na utawala CELG, chini ya ufadhili wa legal services facility kimeibua aina za ukatili unaowakabili wananchi wilayani Kiteto mkoani manyara.

Wakiwa katika mafunzo ya siku tano na wasaidizi wa kisheria wilayani Kiteto, imeelezwa kuwa vitendo vya kikatili vinazidi kuongezeka siku hadi siku, kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo mamlaka za Serikali kutowajibika ipasavyo

Mwanasheria wa kituo cha mazingira CELG, Eliza Maganga alisema, kituo kimebaini kuwepo kwa ukatili katika maeneo tofauti wilayani Kiteto akisema, njia pekee za kukabiliana nao ni kutumia viongozi wa dini, mila pamoja na mamlaka za Serikali kuutokomeza

 Kwa mujibu wa Hassan Konki msaidizi wa kisheria wilayani Kiteto alisema, katika kukabiliana na ukatili huo wilayani Kiteto, miongoni mwa changamoto ni  baadhi ya viongozi wa Serikali, kuwa vikwazo mara ukatili unapotokea kwa kushindwa kuwajibika

Naye Fatua ngao mshiriki katika mafunzo hayo alitaja aina nyingine ya ukatili kuwa ni pamoja na vipigo kwa watoto, ukatili wa kingongo akisema hayo yatatoweka endapo kila mtu  atawajibika katika nafasi yake hasa viongozi waliopewa dhamana na wananchi.

Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wasaidizi wa kisheria 25 wilayani Kiteto ili waweze kuibua ukatili unaofanyika katika maeneo tofauti na kutoa msaada wa kisheria 



Picha kwa hisani ya mwanganamatukio

Maoni