Mwanasheria wa Celg Elizabeth Maganga akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya usaidizi wa kisheria Mohamed Hamad na wenzake 18 Wilayani Kiteto, Manyara, Tanzania..
Kituo cha Sheria za mazingira na utawala, Celg kwa kushirikiana na LSF kutoka Dar eS Salaam, wamewapa vyeti wasaidizi wa kisheria kumi na tisa, Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, kufuatia kufuzu mafunzo waliyopata ya ukatili wa kijinsia
Akikabidhi vyeti hivyo, Elizabeth Maganga mwanasheria wa Celg, aliwataka wasaidizi hao wa kisheria kuhakikisha kuwa wanatimiza wajibu wao wa kuisaidia jamii inayoteseka kwa kukosa elimu ya ukatili wa kijinsia
alitaja mada zilizofundishwa kuwa ni pamoja na majukumu ya msaidizi wa kisheria, kuwajengea uwezo wasaidizi wa kishera jamii, Ushawishi, Haki za Binadamu, haki za wanawake, Jinsia na ukatili wa kijinsia, Ndoa na taratibu zake
Zingine ni Ajira, kazi na hifadhi ya jamii, Mtoto na haki zake, Urithi na mirathi, Rasilimali ardhi, Mazingira na uhifadhi wa mazingira, Haki za raia katika mfumo wa jinai, Uongozi na utawala, pamoja na utunzaji wa kumbukumbu na taratibu za uendeshaji na usimamizi wa ofisi
Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake Hassani Konki alipongeza Kituo cha Celg kwa kushirikiana na LSF kuandaa mafunzo hayo kwaajili ya wasaidizi wa kisheria akisema wameyapata wakati mwafaka ambapo kunachangamoto kubwa za ukatili Kiteto
Kwa upande wa Mwadawa Ally Mshiriki alisema mafunzo hayo yatakuwa na tija kubwa kwao na kwa jamii kwani watayatumia kutatulia changamoto zinazowakabili ikiwemo migogoro ya ardhi ambayo imekuwa tishio kwa wananchi
Awali akizungumza na wasaidizi wa kisheria Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya, Tumaini Kambona akiwa ofisini kwake aliwataka wasaidizi hao kuanza kukabiliana na ukatili wa watoto wa shule kupachikwa mimba ambapo alisema kwa mwezi mmoja uliopita jumla wa wanafunzi 80 waligundulika kuwa na mimba baada ya kupima
mwisho
Maoni
Chapisha Maoni