DC Kiteto, nitatenda haki kwa wakulima,wafugaji




Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa, akifafanua mikakati ya Serikali kuhusu migogoro ya ardhi Kiteto Manyara, Tanzania.

  Lemolo Ole Moringe (mfugaji) akizungumzia mgogoro wa ardhi unavyoathiri Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara Tanzania
Mmoja wa wa wakulima Wilayani Kiteto mkoani manyara Tanzania jina hakutaka litajwe akifafanua sakata ya mgogoro wa ardhi na madhara yake
NA. MOHAMED HAMAD

MKUU wa wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, (DC) Tumaini Magessa, amewahakikishia wakulima na wafugaji, wanaogombania ardhi wilayani humo,kuwa atawatendea haki ili kila kundi linufaike na rasilimali ardhi
Akizungumza  ofisini kwake, Mkuu huyo wa Wilaya alisema, Kiteto inakabiliwa na migogoro ya ardhi kila upande, akidai njia atakayotumia kwa sasa ni kushirikisha makundi ya wakulima na wafugaji katika utatuzi huo
“Mashariki Kiteto tunamgogoro na Wilaya ya Kilindi,Kaskazini tuna tatizo na Wilaya ya Simanjiro, Magharibi Kondoa na Chemba pamoja na Wilaya ya Kongwa ya Dodoma upande wa kusini”
Alisema kila Wilaya ina utaratibu wake, hivyo wananchi wanaohitaji ardhi hasa Kiteto, wanapaswa kufuata taratibu na sio kuvamia kama ilivyo awali kuwa kila mtu alijitwalia ardhi kinyume na utaratibu
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima wilayani hapa walidai kuwa moja ya matatizo waliyonayo ni pamoja na baadhi ya viongozi wa Sererikali kutokuwa waadilifu na kujihusisha na vitendo vya rushwa katika kushuhulikia migogoro hiyo
“Tuna tatizo hapa, migogoro ya ardhi imekuwa vyanzo vya baadhi ya viongozi, na ukitaka kushuhulikiwa na haki itendeke kwa wakulima na wafugaji ambao wanadai kila eneo ni hifadhi ujanjaujanja wa kifedha unaofanywa katika kuanzisha hifadhi zinazoleta migogoro uachwe”
Alisema haiwezekani kila eneo likawa hifadhi, lazima Serikali itende haki katika hili la sivyo kutakuwa na mgogoro usio isha kama ilivyo sasa kuwa viongozi wa wilaya mkoa na Taifa wamefika Kiteto lakini hakuna utatuzi wa wazi,alisema Bakari Maunganya (mkulima)

Posted by mwanganamatukio..

Maoni