Katibu mwenezi CCM na diwani wa kata ya Kaloleni, achomwa mkuki, Kiteto


Katibu mwenezi CCM na diwani wa kata ya Kaloleni, achomwa mkuki, Kiteto

NA. MOHAMED HAMAD
Wilaya ya Kiteto iliyopo Mkoani Manyara, imekuwa na migogoro ya ardhi
kati ya wakulima na wafugaji, hali iliyosababisha  watu kushindwa
kufanya shughuli zingine za maendeleo na wengine kujeruhiwa na hata
kuuawa

Kufuatia migogoro hiyo, baadhi ya idara mbalimbali za Serikali  kama
afya,maji na elimu zilionekana kusuasua  kutokana na  migogoro hiyo
hali iliyosababisha manunguniko makubwa kwa wananchi juu ya Serikali
yao

Hali hiyo ilidaiwa kuwachelewesha sana wananchi kimaendelea, kwa miaka
minne mfululizo, wasijue cha kufanya huku baadhi yao wakipoteza maisha
na wengine kujeruhiwa wakati wakigombea ardhi, jambo lililosukuma
Srikali kuunda tume mbalimbali kuchunguza

Mbali na kupoteza maisha wengi walipata ulemavu wa kudumu, na umaskini
kwa kuteketezewa mali zao zikiwemo pikipiki,  mazao, na kuwafanya
waishi kwa taabu katika maisha yao, hali iliyoilazimu baadhi ya
watumishi wa Serikali kuhamishwa vituo vya kazi

Waliohamishwa ni pamoja na baadhi ya wakuu wa idara, watendaji wa
vijiji  na hata wanasiasa kushindwa kurejea katika nyazifa zao wakati
wa uchaguzi, kufuatia madai kuwa wamechangia migogoro hiyo

Kwa miaka miwili, Wilaya ya Kiteto ilidaiwa kuwa shwari hali
iliyosababisha wananchi wengi kuanza kurejea katika hali zao za
kawaida kwa kufanya shughuli zao za kilimo na wengine ufugaji kwa
lengo la kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao

Utulivu huo ulisababishwa na tume kadhaa zilizoundwa na aliyekuwa
Waziri  Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda, kutaka kujua kiini cha
migogoro hiyo na kuitafutia ufumbuzi ambapo waliweza kufanya kazi kwa
zaidi ya siku sitini

Kwa mujibu baadhi ya viongozi, walieleza chanzo cha migogoro ya ardhi
Kiteto ni kukosekana kwa uadilifu kwa baadhi ya viongozi wa vijiji
ambao wametajwa kuuza ardhi kinyemela kinyume cha sheria ya ardhi
namba 5 ya mwaka 1999

Akizungumza na wenyeviti wa vijiji 68 pamoja na watendaji wao,
Eliakimu Maswi, Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara alisema, Serikali
imebaini chanzo cha migogoro, na kuwataka watumishi kujipima kama
wanaendana na kasi ya magufuli ikiwezekana waache kazi kabla ya
kutumbuliwa

“Tumebaini kuwa wenyeviti wa vijiji na watendaji wao wamekuwa vinara
wa kuuza ardhi, sasa hatuna nafasi ya kuwabembeleza, tutawatumbua na
kuwafikisha mahakamani...hatutamwonea haya mwenyekiti tutawakamata DC
nakuomba watie ndani bila wonga”

Alisema uwezo wa kijiji kutoa ardhi ni ekari 50, zaidi ya hapo ni
wilaya na kiwango cha juu zaidi ni Wizara, inakuwaje mwenyekiti wa
kijiji au kitongoji atoe zaidi ya ekari 1,000, 2,000 na hata 5,000
anapata mamlaka hayo wapi mwenyekiti alihoji Katibu Tawala

“DC, Mkuu wa Wilaya naomba sasa tufanye kazi, na wala usisite
kumchukulia hatua mwenyekiti wa kijiji, muweke ndani haraka unapoona
kuwa amefanya makosa kwa maksudi, kwa kufanya hivyo tutapunguza
uhalifu huu”alisema Katibu Tawala Maswi

Kwa upande wa  Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumain Magessa akizungumza na
viongozi  wa vijiji alisema, amelazimika kuita kikao hicho cha kazi
ili kutaka kuanza ukrasa upya wa kuwavusha salama wanachi wa Kiteto
kufanya kazi bila kubughudhiwa

Wakati kukiwa na mikakati hiyo Diwani wa Kata ya Kaloleni, Wilayani
Kiteto Mkoani  Manyara, Christopher Parmet (CCM), alinusurika kifo
baada ya kuchomwa mkuki na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji wakati
wakiswaga mifugo iliyokuwa imeingia shabani kwake

Tukio hilo limetokea maeneo ya Kisima Kata ya Amei, Wilayani Kiteto,
wakati diwani huyo na wafanyakazi wake, Chibundiki Naisoni (54) na
Harold Mtalima (56) wakiswaga mifugo iliyokuwa imeingia shambani na
kula mazao aina ya mbaazi

 “Baada ya kupigiwa simu na wafanya kazi wangu wa shambani kuwa
ng’ombe  wameingia shambani, nililazimika kwenda  na kuwakuta, ambapo
tulimpigia simu mwenye mifugo ili aje, lakini alikataa akisisitiza
mifugo yake iachiwe mara moja”

Alisema kufuatia hali hiyo alilazimika kuamuru ipelekwe kwa uongozi wa
Kitongoji, na wakati wakiiswaga, ghafta lilijitokeza kundi la vijana
wa kimasai na kuanza kurusha fimbo na mikuki ambapo hapo waliweza
kumchoma mkuki mkono wa kulia na wasaidizi hao kujeruhiwa sehemu
mablimbali za miili yao

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa,  alisema,
alipigiwa simu na Diwani huyo, aliyekuwa akidai anaishiwa nguvu baada
ya kuvuja damu nyingi kwa kuchomwa mkuki  na kuagiza Polisi kwenda
kumchukua

Alisema matukio haya awali yalikoma lakini inaonekana kufanywa na
wafugaji wa Wilaya za jirani na kutoweka ambapo amedai jitihada za
kukabiliana na tukio hilo ni kuwa na daftari la wakazi kila kijiji ili
kuwabaini wahalifu hao

Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian (CCM) alizitaka mamlaka za
Serikali Mahakama na Polisi,  kutimiza wajibu wao ili kukomesha
matukio hayo ambayo aliyaita kuwa ni ya kujirudia kwa kutochukuliwa
hatua madhubuti

Alisema matukio hayo ni mwendelezo wa mauaji yaliyokwisha kufanyika
Kiteto ambapo Wilaya imejipanga kukabiliana na tukio hilo la kihalifu
akisisitiza kuwa kila mamlaka zitimize wajibu wao sambamba na wananchi
kutoa taarifa mapema kukabiliana na matukio hayo ya kikatili

Mwenyekiti wa wenyeviti 68 Wilayani Kiteto, Salimu Mbwegu, akizungumza
kwenye kikao maalumu kilichoitwa mwanzo mpya wa kuirejesha Kiteto
yenye amani, chini ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto (DC) Tumaini  Magessa
alisema, njia pekee ya kukabiliana na migogoro kila mmoja atimize
wajibu wake

“Baadhi ya wenyeviti na wayendaji wao wanalalamikiwa kuhusika katika
migogoro ya ardhi, lakini hivi wenyeviti wanalipwa?..na kwanini
hawalipwa wanafanyaje kazi za Serikali..tunaitaka Serikali kuwalipa
pamoja na kutoa 20% za vijiji ili waweze kujiendesha”

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kiteto, Tamimu Kambona, aliwahakikishia wenyeviti hao kuwa
wameandaliwa malipo yao sambamba na 20% za vijiji japo sio zote ila
wapate cha kuanzia katika maendeleleo ya vijiji

Kambona pia aliwaonya baadhi ya watumishi wa Serikali, kuwa niwalevi
wa kupindukia kuwa hatowavumilia sheria kali itachukuliwa chidi yao,
sambamba na kuwafukuza akidai  utawala huu ni tofauti kwamba hawezi
kuendelea kuwavumilia bila kuwatumbua

Mwisho



Maoni