Kauli ya kocha wa yanga, Pluijm, kabla ya wabishi Mbao FC


Published in Jamii
hans
Na.Alex Mathias,
Dar es salaam.Baada ya kufanyika kazi ya ziada ya kumshawishi Kocha Hans Van Der Pluijm kurejea kuifundisha Yanga anatarajia kusimama kwenye benchi la ufundi dhidi ya wabishi wa Mwanza Mbao FC kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Pluijm raia wa Uholanzi aliamua kuandika barua kuachia ngazi, lakini uongozi wa Yanga ukamuangukia na kumfanya abadili uamuzi wake huo.
“Najua itakuwa mechi ngumu, timu zote zinajiandaa na inakuwa faraja kwao kushinda dhidi ya Yanga ambao ni mabingwa kwani niliwaona kwenye mechi yao na Simba waliwakomalia”alisema Pluijm.
Aidha amesisitiza kuwa Wachezaji wangu wako tayari na wanajua sisi ni kina nani na wanaocheza na sisi wanataka nini tutaingia kwa kauli moja tu ni kupata alama tatu muhimu kwani hakuna kulala.
Yanga imeonyesha kurejea katika kiwango chake kwa kushinda mabao kumi katika kila mechi, ikianza na kuitandika Kagera Sugar mabao 6-2 na JKT Ruvu mabao 4-0.
Na mpaka sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na alama 24 kwa michezo 11 na ikizidiwa alama 8 na vinara Simba wenye alama 32 mechi 12.(P.T)

From mjengwa blog..

Maoni