Ramani ya Simanjiro Manyara. |
Ili kuepusha kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi, halmashauri ya wilaya ya Simanjiro,Mkoani Manyara imejipanga kikamilifu kuhakikisha inaondokana kabisa na migogoro hiyo, ambapo kesi zote za ardhi zitatatuliwa na mabaraza ya ardhi ya kijiji na kata bila kuingiliwa na watendaji ,wanasiasa, na wenyeviti ambao wameonekana kuingilia migogoro hiyo badala ya kuyaachia mabaraza husika kushughulikia utatuzi huo.
Ngazi ya chini kuna mabaraza ya ardhi ya kijiji na kata ambayo yapo kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi,ambayo yamepewa dhamana ama jukumu la kukaa na kutatua migogoro hiyo bila kuingiliwa na watendaji, wanasiasa, wenyeviti , madiwani ili kuweza kuleta ufanisi> katika utendaji wa kazi zao,hali inayosababisha kuwepo na kuongezeka kwa migogoro mingi inayopelekea hata vifo kwa raia.
Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro,Mkoani Manyara Yefred Myenzi, alipokua akiongea kwenye baraza la madiwani lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo, ambapo alisema tayari halmashauri yake imekwishatoa mafunzo maalum ya kila kiongozi kutambua majukumu na mipaka ya kazi anazotakiwa kufanya, hivyo ategemei kuona mwiingiliano wa majukumu hayo yakiendelea.
Myenzi alisema kamwe kukiwa na mwingiliano wamajukumu yoyote yale, itakua ni vigumu kufikia muafaka wa jambo husika, kwani vipingamizi vitakua vingi vya kupinga jambo husika,hivyo ni vema kuepukana mapema na migongano ya majukumu na hata mwingiliano wa wajibu kati ya watendaji wa vijiji na kata, wenyeviti wa vijiji, wanasiasa ,watoa maamuzi ya haki, na madiwani kutojihusisha kabisa na utatuzi wa migogoro ya ardhi na badala yake wayaachie mabaraza ya ardhi ya kijiji na kata katika kukabiliana na changamoto hiyo na si vinginevyo.
"Waheshimiwa madiwani nyie kama wasimamizi wakuu wa shughuli za maendeleo katika kata zenu hivi mtajisikiaje pale mtakapoona viongozi wengine wanakuja kuingilia majukumu yenu, mtajisikiaje,hivyo Kila mmoja wetu ahakikishe anawajibika kikamilifu katika majukumu yake, bila kuingiliwa na mtu yaani kila mmoja atambue kipaka ya kazi zake,kwa kufanya hivyo tutakua tumeendana na taratibu,kanuni na sheria zetu ha nchi" alisema Myenzi.
Aidha alisema iwapo kuna mabaraza ya ardhi yasiyofanya kazi basi ni muda muafaka wa kuhakikisha yanaundwa upya ,yaliyokuwepo yaimarishwe ili yaweze kufanya kazi kikamilifu ndani ya mwezi oktoba,2016, kwa mujibu sheria.
"Naomba hili lifahamike waheshimiwa madiwani,usuluhishi wa migogoro ya ardhi kwa njia ya kimila naomba usiingiliane kabisa taratibu za kisheria zilizowekwa kwa mujibu wa sheria za ardhi,kwani mabaraza ya ardhi yapo kwa ajili ya kutoa maamuzi ya haki kwa Kila> mmoja,hivyo yasiingiliwe yameundwa kwa mujibu wa sheria tuyaachie tafanye kazi zao kwa uhuru" asisitiza Myenzi.
Maoni
Chapisha Maoni