Walengwa wa TASAF waishukuru Serikali



Baadhi ya walengwa katika mradi wa jamii TAFAS Kijiji cha Engusero,Wilayani Kiteto mkoani Manyara Tanzania, katika moja ya kikao cha kupewa ruzuku ya kujikwamua na umaskini inayotolewa na serikali kila mara..


Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Kanali Samuel Nzoka akiwa katika zoezi la ugawaji wa ruzuku ya Serikali kupitia mradi wa jamii TASAF Kijiji cha Engusero..

Nicodemus John aliyekuwa katibu Tawala Wilaya ya Kiteto ambaye amehamishiwa Hai akiwa katika zoezi la ugawaji wa ruzuku ya Serikali kwa kaya maskini kupitia mradi wa jamii TASAF Kijiji cha Engusero..

Serikali hapa nchini, imebadilisha mfumo wa kukabiliana na umaskini kwa kuwapa fedha keshi wananchi wake, tofauti na awali ambapo waliweze kuelekeza fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo

Awali fedha hizo zilielekezwa kwenye miradi ya maji, afya, barabara, pamoja, na elimu, na kuwafanya wananchi wengi kunufaika tofauti na ilivyo sasa kuwa kaya maskini ndizo zilizolegwa katika miradi hiyo

Kufuatia hali hiyo walegwa wa TASAF kwa nyakati tofauti wanapofikiwa na ruzuku hiyo wamekuwa wakiishukuru Serikali kwa kuwapa fedha keshi kwaajili ya kujikimu kimaisha

Philipo Sengela ni mratibu wa TASAF wilaya ya Kiteto mkoani Manyara Tanzania, alisema fedha hizo zimekuwa na msaada mkubwa kwa walengwa, wengi wao kusomesha watoto, kuanzisha miradi pamoja na kujikumu kimaisha...



Maoni