DED Kiteto aonya watumishi wezi..


DED Kiteto,Tamimu kambona, akizungumza na madiwani pamoja na wakuu wa idara hivi karibuni...
Diwani Hassan Benzi wa kata ya Dosidosi (CCM) akiwa na wenzake katika moja ya kikao cha Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto..

 Afisa mipango wa Wilaya ya Kiteto Bw. Malley katika na wenzake, kikao cha baraza la madiwani Kiteto..

MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Mkoani
Manyara, Tamimu Kambona, ameonya baadhi ya watumishi kuacha kuiba
fedha za Serikali.

Kambona ametoa kauli hiyo jana kuwa baadhi ya watumishi wa Serikali
wanatumia nafasi zao, kuhujumu mapato ya halmashauri kwa manufaa
binafsi.

"Halmashauri tuna chanzo chetu cha mapato, ushuru wa mkaa,sasa baadhi
ya wenzetu tuliowapa nafasi ya kukusanya wanafanya watajavyo..hili
halikubaliki"

Alisema katika hujuma hizi, amegundua kuwa kibali kimoja cha
kusafirisha mkaa kinatumiwa kusafirisha zaidi ya gari moja, akidai
analazimika kufuatilia wakati mwingine na kubaini hayo

Nilimfukuza kazi mtumishi mmoja juzi..yeye aliandikia gari kibali cha
tsh 75,000 wakati fedha halisi ilikuwa laki 750,000, hatuwezi
kuendelea kwa kuwa na watumishi wa aina hii.."alisema Kambona huku
akionyedha kuchukizwa

Alisema ataendelea kuwafukuza kazi kutokana wenye tabia hizo, akidai
hajutii kufanya hivyo, kutokana na mfumo uliopo kuwa atakayefanya kazi
Serikalini ni yule mwenye uwezo wa kuendana na kasi hiyo

Uchunguzi uliofanywa na Jambo Leo, umebaini kuwa watumishi hao
wanajihusisha na tabia hizi kutokana na baadhi ya madiwani kuwalinda
wa wakionekana na makosa

Hali hii inatokana na mgawanyiko wetu sisi madiwani, Leo utataka kujua
juu ya mtumishi anayetuhumiwa miongoni mwetu wanajitokeza madiwani
na,kumtetea, alisema Kidawa Othuman Iyavu diwani wa kata ya Matui
Chadema

Nao baadhi ya wananchi waliozungumzia sakata hili walusema, wamefanya
makosa awali kuwachagua madiwani wenye dhamira ya kujinufaisha Wao
badala ya wananchi

"Hapa tumepoteza..kumtoa diwani aliye madarakani ni,kazi,kubwa Sasa
tujipange tu kipindi,kijacho kuona Kama tunaweza kumpata kiongozi
mwrnye maslahi na,umma"alisema Bakari Maunganya mwananchi

Mwisho

Maoni