TFDA wafunga machinjio Kiteto..

Picha ya machinjio hapa nchini ambapo Serikali iliweza kuchukua hatua kwa kufunga..
Biashara ya nyama baadhi ya maeneo hapa nchini..

NA. MAOHAMED HAMAD
Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) kutoka mkoani manyara, imezuia
wafanyabiashara wa nyama Wilayani Kiteto, kutofanya biashara hiyo,
hadi wajengewe machinjio kama sheria na taratibu za afya
zinavyoelekeza

Wilaya ya Kiteto haina machinjio, hivyo wafanyabiashara walilazimika
kutoka nje ya mji wa Kibaya kufuata jengo la machinjio lililopo km
moja kutoka mjini, ambalo limedaiwa kutokuwa na maji, choo, shimo la
taka na uzio

Akizungumza hayo, Jackob Barnabas, Afisa wa TFDA mkoani Manyara,
alisema amelazimika kuzuia biashara hiyo kufuatia hofu ya kuibuka
magonjwa yatokanayo na uchafu unaozalishwa na biashara hiyo ya nyama

Alisema pamoja na maelekezo aliyotoa mwezi wa tano mwaka 2016, kumtaka
Mkurugenzi kujenga machinjio ya Wilaya, hakuna hatua zilizochukuliwa,
huku kukiwa na hofu kubwa ya kuibuka kwa magonjwa ya maambukizi

“Ili kulinda afya za wananchi wa kiteto.. nimelazimika kuzuia
wafanyabiashara wa nyama wasiendelee na biashara ingawa najua madhara
yake, lakini kuna kila sababu ya kutazama madhara makubwa yanayoweza
kujitokeza yakiwemo maafa” alisema Afisa huyo wa TFDA

Baadhi ya wafanyabiashara wa nyama walisema, pamoja na kulalamika kwa
muda mrefu juu ya eneo hilo ambalo halina hadhi ya machinjio,
waliendelea kutozwa ushuru bila kufanyika  maboresho yoyote katika
jengo hilo

Wakizungumza hayo, Ismail Mohamed, na Mnuo walisema, mbali na madhara
ya kiafya yanayoweza kujitokeza kwa wananchi kutokula nyama, kiuchumi
wao wataathirika, hasa wafanya biashara wa hotelini na mama lishe
ambao huwa msaada mkubwa kuuza vyakula mitaani

“Pale hatuna maji, choo, uzio, shimo la taka na huwa tunalazimika
kuagiza akinamama wanaochota maji korongo la mnadani kutuletea ili
tuweze kufanya biashara ya nyama mjini Kibaya”alisema Ismail Mohamed
(mfanyabiashara wa nyama)

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, Tamimu
Kambona, alikiri kuwapokea maafisa hao wa TFDA akisema,  aliruhusu
wafanye kazi ya ukaguzi na mara baada ya kumaliza kazi yao watampa
mrejesho

Nitakapopata raarifa rasmi ya kimaandishi nitajua cha kufanya..ndio
kwanza unaniambia kuhusu hili, najua kuna uzembe mkubwa wa wasaidizi
wangu kutonipa taarifa mapema na hapa naelekea vijijini kwahiyo
sitaonana nao ingawa najua hali ni mbaya ya machinjio yetu alisema
Kambona

MWISHO

Maoni