Kero ya maji Kiteto itaendelea mpaka lini?













NA. MOHAMED HAMAD
Wilaya ya Kiteto ilizinduliwa mwaka 1974, wakati huo kulikuwa na idadi
ya watu 12,000, kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012,
idadi ya watu iliongezeka na kufikia zaidi ya 240,000.

Wakati wilaya  inazinduliwa  maji yalitosha kulingana na idadi ya
watu, waliweza wafanya  shughuli za maendeleo, tofauti na ilivyo sasa
kuwa wanalazimika kutumia muda mwingi kutafuta maji kuliko kufanya
shughuli zingine

Hali hii imekuwa tishio kwa familia na wananchi Wilayani Kiteto, hasa
wa vijijini ambao vipato vyao vinaishia kununua maji, huku kukiwa na
mahusiano mabaya kati ya wanandoa kufuatia kutoaminiana wakati
wakisaka maji

Kesi za wanandoa zinaongezeka siku hadi siku kipindi hiki, kutokana na
tatoaminiana kwao, mtu unalazimika kuamka saa 10 za usiku kwenda
kuweka foleni na upatikanani wa maji huwezi kujua kufuatia uhaba huo,
alisema majabu Zuberi (mwananchi) wa Kijiji cha Kijungu

Viongozi wilayani Kiteto wamekuwa wakilalamikiwa kwa kushindwa
kusogeza huduma ya maji karibu na wananchi, huku kukiwa na ahadi
zisizotimilika kuwa Serikali iko mbini huku wilaya  ikiwa na uwezo wa
kujimudu kwa maji safi na salama vijijini kwa 36% na mjini 37%

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa miundombinu inayotumika bado ni ile
ya mwaka 1974 wakati wilaya inaazinduliwa kama matenki na mabomba
pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali kuondoa adha hiyo bado
hali hiyo imekuwa tishio

Wakati huduma hiyo ikihitajika urasimu umetajwa kuwa kikwazo ambapo,
aliyekuwa Makamu wa Rais Dr.Ally Mohamed Shein ambaye kwa sasa ni Rais
wa Zanzibar, aliwai kuzindua tanki hewa la maji lenye lita laki tatu
mjini Kibaya, kuwa limekamilika

Lengo la uzinduzi huo lilikuwa ni kuonyesha uongozi huo kuwa kero ya
maji mjini Kibaya  itakuwa imekwisha, kwani taarifa za uhakika
zinaeleza siku hiyo maji yalienda kuletwa kwa boza na kumiminwa ndani
ili uzinduzi ufanyike

Kwa mujibu wa taarifa za mradi huo gharama za mradi huo ujenzi wa
matengi mawili ya kisasa maashine pamoja na mambomba zilikuwa ni mil
200 ambapo hadi leo huduma hiyo haipatikani kupitia mradi huo huku
kukiwa hakuna majibu yaliyotolewa na Serikali ya Kiteto juu ya mradi
huo

Katika hatua hiyo kwa hali ya uwajibikaji, wananchi walitamani kuona
hatua zikichukuliwa juu ya  baadhi ya viongozi waliohujumu mradi huo,
lakini kutokana na kile kilichoitwa kuwa ni kulindana, madhara
yameendelea kujitokeza siku hadi siku na asichukuliwe hatua mkosaji

Ndoo moja ya maji vijijini huuzwa sh 500 mpaka 700 huku maeneo ya
mijini ikiuzwa sh 100 hadi 300, hali inayodaiwa kuwafanya wananchi
kushindwa kufikia malengo yao kwa kutumia muda na fedha kwa maji
kuliko shughuli zingine za maendeleo

Katika kuonyesha ukubwa wa tatizo hilo Mbunge wa viti maalumu Manyara,
Esther Mahawe (CCM) alilazimika kuangua machozi kumtaka naibu Waziri
wa maji kuja kutembelea maeneo ya mkoa wa Manyara kujionea hali ilivyo

Naibu Waziri wa Maji na Umwagilianji Mhandisi, Isack Aloyce Kamwelwe,
na Mbunge Jimbo la Katavi, alipofika Kiteto alimtaka Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya, Tamimu Kambona, kuwasilisha hati (certificate)
za utekelezaji wa miradi ya maji ndani ya siku mbili, ili wapate
malipo ya kukamilisha miradi kuondoa adha iliyopo

Hatua hiyo imefikiwa, kufuatia ombi maalumu lililofanywa na Mkurugenzi
Mtendaji  wa Halmashauri ya Kiteto, kuhusu ongezeko la gharama za
mradi, kutoka kwenye mkataba wa awali hadi kufikia kiasi cha tsh mil
39,681,000 kukamilisha miradi hiyo

Alisema lengo la Serikali ni kutekeleza sera ya kuwa wananchi
wayafikie maji mita 400 pawe kituo, akisema kwa sasa makusanyo
yameongezeka, sambamba na kuzuia mianya ya wizi Serikali hivyo kuna
uwezekano mkubwa wa kufikiwa Sera hiyo ambayo kila mtanzania
anatufaika nayo

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Kambona, miradi ya maji mjini Kibaya na
Kaloleni, imetekelezwa kwa asilimia 75, ambapo kazi zilizofanyika ni
usanifu wa mradi, kufungwa mfumo wa nishati ya jua, kufungwa pamp
moja, kulazwa mabomba na kufukiwa mitaro

Mradi mwingine ni wa umwagiliaji uliopo Kijiji cha Orgira Kata ya
Sunya, ambao umefikia hatua za mwisho za utekelezaji uchimbaji wa
kisima ulikamilika, ufungaji wa pamp, ulazaji wa mabomba, ujenzi wa
vituo vya kuchotea maji, ujenzi wa kituo cha kunyweshea mifugo, pamoja
na ujenzi wa tanki la maji na miundombinu yake

Mkurugenzi huyo alimhakikishia Naibu Waziri huyo kuwa, atatekeleza
agizo hilo haraka, kwani kuna uhitaji mkubwa wa fedha hizo ili
kukamilisha miradi ambayo kwa sasa wananchi wanapata adha kubwa ya
maji, kwa kuwa ilikuwa inatumia mifumo ya jua na kwamba,
linapokosekana upatikanaji wa maji huwa mgumu

Akizungumza ukubwa wa tatizo la maji Wilayani Kiteto na mkoa wa
Manyara kwa ujumla, Mb. wa Viti Maalumu, Esther Mahawe alisema,
Serikali haina budi kutatua kero ya majini hasa vijijini kwani hali ni
mbaya kwa wananchi wanatumia muda mwingi kutafuta maji kuliko kufanya
shughuli zingine za maendeleo

“Kama unakumbuka Mhe. Naibu Waziri, nilipofika kwako kukuomba kuja uje
ujionee hali ilivyo vijijini nililia kwa uchungu…na wewe ukaniahidi
kuwa utakuja nisema tu umejionea hali ilivyo, sasa tunaomba msaada
wako ili uwatue ndoo ya maji akina mama wa Kiteto na Manyara kwa
Ujumla wanaotaabika kila kukicha”

Kwa Upande wake Emmanuel Papian Mbunge wa Jimbo la kiteto, aliomba
Serikali kuendelae na jitihada za kusogeza huduma za jamii karibu na
wananchi ili wananchi wawe na imani na viongozi wao waliopo
madarakani, na kuwasihi wananchi kutunza miradi katika maeneo yao

Alisema kukosekana kwa vyanzo vya maji vya uhakika, kumepelekea uhaba
mkubwa wa maji, ambapo visima vingi vinapochimbwa,maji  hayakupatikana
na kuomba wataalamu wa maji waliobobea kuona haja ya kuja Kiteto
kusaidia wananchi hao ambao wanataabika

Kwa mujibu wa taarifa Wilayani hapo  vyanzo vya maji vilivyopo ni
visima virefu 74, visima vifupi 8, chemchemu 6, mabwawa makubwa 5,
mabwawa madogo 36, na matengi ya kuvunia maji ya mvua 80, ambapo
huduma ya maji safi na salama vijijini inapatikana kwa 36%

Baadhi ya wananchi Asha Issa wa (Kaloleni) Elias Kona (Kijungu) na
Diwani Mandalo Abdillahi, waliiomba Serikali kuhakikisha inatatua kero
ya maji hasa katika kipindi hiki, kutokana na ukubwa wa tatizo hilo
ambalo linawagharimu na kushindwa kuendesha maisha yao

Katika hatua hiyo kumekuwepo na ahadi nyingi zinazotolewa na viongozi
wa  chama na Serikali kufuatia uhaba wa maji, ambapo Ismail Kaboja
(mwanchi) alisema zimekuwa hazitimiliki huku adha hiyo ikiendelea

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Dongo, Elia Dengea (CCM) alisema,
kuna kila sababu ya kufanyika utaalamu kwa kina katika maeneo ya
Kiteto hasa kata yake ambako walichimba maji zaidi ya mara sita chini
ya watu wa misri bila kufanikiwa kupata maji

Alisema hali hiyo imekuwa tatizo kubwa ambapo hakuna mwananchi
anayemwamini kiongozi anachosema, huku wtakutana kipindi cha uchaguzi,
ambapo watafanya mabadiliko ya uongozi baada ya kudanganywa kwa muda
mrefu

Naye Kidawa Othmani Diwani wa kata ya Matui Chadema alisema, tatizo
lililopo ambapo kwa sasa linagharimu wananchi kuhusu sekta ya maji ni
kukosa watumishi wa Serikali ambao ni waadilifu akisema kuna hujuma
nyingi zimefanyika hakuna hatua zilizochukuliwa

Alisema katika eneo lake la kata wananchi wanatumia maji ya visima
vifupi vya kuchimbwa kwa mkono huku kukiwa na Serikali iliyowaahidi
wananchi huduma za jamii jambo ambalo amedai anachofanya ni kueleza
ukweli wananchi juu ya kinachofanyika ili waamue wenyewe

“Nimekuwa nawaambia wananchi kuwa hii ni Serikali ya chama cha
Mapinduzi, sasa waamue kunyoa ama kusuka, ila kwa sasa ni kama kuna
matumaini baada ya kuingia John Pomber Magufuli, labda anaweza
kurekenisha kama hatohujumiwa kama tunavyoona

Mwisho


Maoni