Mbaroni kwa kupachika mimba wanafunzi 3

                                        Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis Massawe

WATU watatu Wilayani Kiteto, Mkoani Manyara, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani hapo, kwa tuhuma za kuwabaka na kuwapa mimba wanafunzi watatu wa shule ya Sekondari ya Kiteto

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Manyara Francis Massawe, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Elihuruma Benjamini (30), Yona Mtambo (30) na Rajabu Hajji (18) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Bwakalo iliyopo kaya ya kaloleni,  aliyempa mimba mwanafunzi wa Kiteto Sekondari

Kwa mujibu wa kamanda Massawe alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na zoezi la upimaji mimba kwa wanafunzi wa kike lililofanywa na uongozi wa shule ya Seokondari Kiteto

“Watuhumiwa tunakusudia kuwafiukisha mahakamani wakati wowote kuanzia sasa, na wanafunzi tutaendelea kuwashikilia mpaka tutakapowafikisha mahakamani watuhumiwa hao”alisema kamanda  Massawe

Akiongea na MTANZANIA mmoja wa waalimu wa shule ya Sekondari Kiteto ambaye hakutaka kutaja majina yake, alisema toka mwanzo wa mwaka huu hadi Sept 15 2016, jumla ya wanafunzi wa kike tisa wamegunduliwa kuwa na ujauzito

Wanafunzi waliopata ujauzito ni kati ya kidato cha pili na cha nne, ambapo hapo shuleni huwa kila mara wanautaratibu wa kuwapima wanafunzi wa kike ili kudhibiti mimba shuleni, hali inayodaiwa kuwa tishio Wilayani hapo

Hatua hiyo imefikiwa, kufuatia msisitizo wa kudhibiti mimba shuleni kutoka kwa uongozi wa Wilaya na hata viongozi wa dini ambao wamekuwa na kampeni ya kukemea matukio hayo na kuitaka Serikali kutokomez

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa, hivi karibuni akizungumza na wakazi wa mji wa Kibaya aliwahakikishia kuwa Serikali itaanza kuwachukulia hatua wanaojihusisha na kuwapa mimba wanafunzi

Kwa upande wa baadhi ya wananchi waliozungumzia sakata hili walisema, kukithiri kwa mimba shuleni kumetokana na baadhi ya wazazi kushindwa kuwahudumia watoto wao, na wanafunzi hao kuchukua jukumu la kulisha familia zao

MWISHO

Maoni