NMB Kibaya watoa msaada vitanda, madawati wa mil 15

 Meneja wa benki ya NMB kanda ya kati, Straton Chilongola,akitoa taarifa kwa Uongozi wa Wilaya ya Kiteto namna Benki ya NMB Kibaya ilivyochangia maendeleo wilayani Kiteto mkoani manyara..





 Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kati, Straton Chilongola,akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa, dawati moja kati ya madawati 100 waliochangia NMB Kibaya za thamani ya mil 10 kama moja ya jitihada za kuisaidia Serikali ya Kiteto mkoani manyara..





Mkurugenzi wa kiteto Tamimu Kambona wa pili kushoto na meneja wa Benki ya NMB Kibaya Bw. Said wakishuhudia makabidhiano ya madawati yaliyotolewa na NMB Kibaya
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona, akimkabidhi Mkurugennzi vitanda 9 vya thamani ya mil 5 alivyokabidhiwea na NMB Kibaya..



 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kiteto, Tamimu Kambona akimkabidhi Mkanga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya Dr Lupembe vitanda vilivyotolewa na NMB Kibaya..

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

 NMB tawi la Kibaya, Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, imetoa
msaada wa madawati 100 na vitanda 9 kwaajili ya wagonjwa katika
hospitali ya wilaya ya kiteto vyenye thamani ya tsh mil 15.

Akikabidhi msaada huo kwa (DC) Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Meneja wa
benki ya NMB kanda ya kati, Straton Chilongola, alisema wamekuwa
wakishiriki shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kusaidia sekta ya
elimu, afya na hata majanga yanapojitokeza

“Mhe. Mkuu wa Wilaya, tumetoa madawati 100 kwa shule za msingi mbili,
Emart na Ngarenaro Wilayani hapa, yenye thamani ya mil 10, vitanda
tisa na magodoro yake vya thamani ya mil 5 kama moja ya jukumu letu”

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa, akipokea msaada huo
alisema, umefika wakati mwafaka ambao wanafunzi  wanatakiwa kukaa juu
ya dawati kama ilivyo agizo la Serikali la kuondoa kero ya madawati
shuleni

NMB mmekuwa msaada Kiteto, mbali na huduma mnayotoa ya kifedha,
mchango huu Serikali tunauthamini, na muendelee kuwa na moyo huo wa
kurejesha faida mnazopata kwa wananchi jambo ambalo ni jema,alisema
DC, Magessa

Katika makabidhiano hayo Mkuu huyo wa Wilaya, alimkabidhi  mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya Wilaya, Tamimu Kambona, na kumtaka
ahakikishe unatumika ipasavyo, ili kuleta tija kwa jamii kama
ilivyolengwa na wadau hao

Kwa upande wake Mkanga mkuu wa hospitali ya Wilaya ya Kiteto Dr.Fracis
Lupembe, alishukuru wadau wa NMB Kibaya akisema, awali walikuwa na
hitaji la vitanda 160 na sasa wamekuwa na jumla ya vitanda 110 hivyo
bado wanaupungufu

Alisema hospitali inakabiliwa na changamoto nyingi zakiwemo
majengo,kutokuwa cha chumba cha maabara chenye hadhi, pamoja na baadhi
ya vitendea kazi na kuomba wadau wengine kujitokeza kusaidia
kuondokana na changamoto hizo

mwisho

Maoni