“Kwanza napenda kumshukuru Mungu. Nimetoka Kenya kuja kutafuta hii pesa
na nimeipata, hivyo namshukuru Mungu. Nawashukuru mabeste wangu wote, na
wote walionipa sapoti. Asante pia Babu.” Alisema Olive huku akitoka
machozi baada ya kutangazwa mshindi.
Hii ni mara ya kwanza kwa taji hilo kwenda nje ya Tanzania ikiwa ni
msimu wa tano toka mashindano haya yaanze mwaka 2009. Olive anakua
msichana wa pili kujishindia taji hilo baada ya Bernick Kimiro
aliyeshinda mwaka 2012.
|
Olive Kiarie, mshiriki kutoka nchini Kenya ameibuka mshindi wa Maisha
Plus East Africa 2016 na kujishindia kitita cha Tzshs. Milioni 30.
|
Shindano la Maisha Plus lilijumuisha washiriki 30 kutoka nchi tano za
Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda ambapo washiriki 16 tu ndio
waliofanikiwa kuingia fainali.
Washiriki Aloyce Sambuta, Irene Ishengoma, Alex Essau, Ngenda Pilly,
Nibigira Baswari, Grace Pemba, Denaice Machocho, Umubyeyi Solange,
Assimwe Marvin, Salmin Omary, Rukia Athuman, Mike Curtywer, Yasinta
Mrisho, Karekezi Jean na Namita Cherrie walifanikiwa kuingia fainali
ambazo zilirushwa jana usiku na kituo cha televisheni cha Azam Two.
[caption id="attachment_148" align="alignnone" width="742"]
Washiriki walioingia Top 5 ya Maisha Plus kutoka kushoto: Aloyce
Sambuta, Alex Essau, Olive Kiarie, Irene Ishengoma na Ngenda
Pilly.[/caption]
Katika hatua nyingine washiriki wanne walipewa tuzo. Aloyce Sambuta
alipata tuzo ya Rais bora na kupewa jumla ya Tshs.Laki nne, Ngenda Pili
alipata tuzo ya mshiriki mwenye heshima kubwa, Mike Cutywer alipaza tuzo
ya mshiriki mdogo wa kiume wakati Namita Cherrie alipata tuzo ya
mshiriki mdogo wa kike.
[caption id="attachment_150" align="alignnone" width="742"]
Top 3 ya Maisha Plus Aloyce Sambuta, Olive Kiarie na Irene Ishongoma[/caption]
Wasanii Ommy Dimpoz na Joh Makini walitoa burudani wakati wa fainali hizo.
From Matukio Daima..
Maoni
Chapisha Maoni