Serikali Kiteto yatatua mgogoro wa ardhi


                                      Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto, Ndaki Stephano

SERIKALI wilayani Kiteto mkoani Manyara, imefuta tangazo la siku saba
kwa wakulima 1561 wa kitongoji cha Onjaniodo lililotolewa na kijiji
cha parimbo la kuzuia shuhuli za kilimo maeneo ya Ndirangoo


Akizungumza mbele ya wananchi wa kitongoji cha Onjaniodo, katibu
tawala wa wilaya ya Kiteto, Ndaki Stephano akiwa na kamati ya ulinzi
na usalama, aliwataka wananchi hao kurejea kufanya kazi ya kilimo kwa
kuwa wako sahihi kufanya shughuli hiyo

"Ndugu zangu wakulima na wafugaji, hakuna mtu bora zaidi ya mwingine
humu, kazi ya serikali ni kuhalikisha kila mmoja wetu ananufaika na
fursa hii ya ardhi"

Alisema katika hali ya kawaida, kitendo kilichofanywa na uongozi wa
kijiji cha partimbo hakikubaliki, kwani huwezi kumtoa mtu aliyekaalia
ardhi miaka mingi kwa tangazo la siku sana na badala yake walipaswa 

kushirikisha juu ya mpango wao huo

Wakumima endeleeni na shughuli za kilimo, na ninyi wafugaji endeleeni
na shughuli za ufugaji mpaka mtakapowezeshwa kupanga matumuzi bora ya
ardhi alisema Katibu huyoTawala Ndani

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya Kiteto, Tamimu
Kambona, aliwaelewa wananchi hao kuwa matatizo mengi yanasababishwa na
baadhi ya wenyeviti wa vijiji kwa maslahi binafsi

Alisema pamoja na,kutoa maelekezo kwa wenyeviti 68 wa vijiji hivi
karibunu ili waweze kuwa na ufahamu wa utendaji wao wa kazi bado
wamekuwa  na matatizo kwa wananchi wao

"Nitakachofanya nikufuata sheria kuondolewa madarakani..siwezi 

kuendelea kuvumilia hii hali, hatufanyi kazi maofisini kazi ni migogoro
 ya ardhi Kiteto,wakati kuna shughuli zingine wa maendeleo za kufanya

Kwa upande wa Abdallah Kishome mwenyekiti wa kitongoji cha Onjaniodo
alisema, hawakuwahi kupanga matumizi ya ardhi na,badala yake maamuzi
hayo yamekuwa yakifanywa na mxenyekiti

Nao baadhi ya wananchi wa kitingoji hicho Meshack Kilapupo (mfugaji)
Richadi kalunjuu (mkulima) walisema, kinachosumbua Wilaya ya Kiteto ni
baadhi ya mashirika ambao wanafanya matumizi ya ardhi bila
kushirikisha wananchi

Wameitaka Serikali kuhakiki mashirika hayo na kazi zao kwani migogoro
mingi ya ardhi Kiteto imechangiwa na mashirika hayo, ambayo
yanajihusisha na matumizi bora ya ardhi

Mwisho

Maoni