Watano mbaroni mgogoro wa mpaka Kiteto, Kilindi

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara Francis Massawe akiwa eneo la Tukio mpakani mwa Wilaya ya Kiteto na Kilindi

JESHI la Polisi wilayani Kiteto, Mkoani Manyara, linawashikilia watu watano, wa kijiji cha Mafisa, Wilayani Kilindi mkoani Tanga, kwa tuhuma za kuchoma moto gari aina ya Noah, lenye namba za usajili T 943 CAK, mali ya Saruni Saninyu (32) mkazi wa kijiji cha Lembapuli

Kamanda wa Polisi mkoani Manyara, Francis Massawe, amethibitisha kukamatwa watu haoi, akisema hayupo tayari kuwataja majina kuhofia kuharibu uchunguzi, na kusema Jeshi la polisi litaendelea kuwasaka watu wengine zaidi waliohusika katika tukio hilo

Alisema awali wananchi hao walifika katika eneo lililopo mpakani mwa Wilaya ya Kiteto na Kilindi na kuamua kuweka mpaka wao, kufuatia kuukataa mpaka uliowekwa na tume ya Waziri Mkuu hivi karibuni, waliofika kubainisha mipaka kuondoa mgogoro baina ya pande hizo

“ Ninachojiuliza kama mpaka ulitakiwa ni nani alipaswa kuweka ..na anayeweweka mpaka ametoka ngazi gani… ili utambuliwe wapi…”alisema kamanda Masswe wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kiteto na Kilindi kufuatia mgogoro huo

Kufuatia hali hiyo Kamanda Massawe alishangazwa na na baadhi ya viongozi waaliopewa mamlaka na na Serikali kushindwa kuchukua hatua mara yanapojitokeza matatizo, na huku wajijitetea kutupia lawama wenzao wanaochukua hatua dhidi ya vitendo vya kihalifu kutoka Kiteto

Alisema kitendo cha kuchomwa gari, wananchi kuamua kuweka mpaka wa mkoa na mkoa, inatosha kuwa lilikuwa ni kosa kwanini watu hawa hawakukamatwa, nani alipaswa kuchukua hatua, badala yake uongozi wa Kilindi wamebaki kulalamika kukamatwa watu wao

“Akizungunza mbele ya kamati ya Ulinzi na usalama za Wilaya ya Kiteto na kilindi, Katibu Tarafa wa Tarafa ya Kwekivu, Mgaya Nyange, alisema kinacholalamikiwa na wananchi wa Kilindi ni kukamatwa hovyo  wananchi wa Kilindi na Polisi wa Kiteto, na ndio maana wameamua kuchukua hatua mikononi”

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashaurri ya Kiteto, Tamimu Kambona, alisema kitendo kilichofanywa na baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Kilindi kuamua kuweka mpaka wao baada ya kukataa uliowekwa na tume ya Waziri Mkuu ni ishara tosha kuwa uongozi umeshindwa kuwasaidia kisheria

Naye (DC) Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Sauda Salum Mtondoo, alimweleza Kamanda Massawe kuwa, lalamiko la wananchi wa Kilindi pamoja na kumhitaji Waziri Mkuu Kassimu Mjaliwa kufika juu ya Mipaka hiyo, tatizo la kukamatwa holela kwa wananchi na polisi kutoka Kiteto sio sahihi

Kwa mujibu wa kamanda masawe, alisema kila mtu haswa kiongozi aliyepewa mamlaka  ana haki ya kukamata anapoona kuna uhalifu kisha kutoa taarifa sehemu husika jambo ambalo alidai, kwa uongozi wa Kilindi wanaona kuwa bado hilo ni kosa na kuwataka watangulize maslahi ya nchi mbele

“Hivi Mkuu wa Wilaya ukihamishiwa kwenda Kiteto leo utakuwa na wazo hili hili kuwa wananchi wa Kilindi wanaonewa, au nyiwe wa kiteto mkija Kilindi mtakuwa na wazo tofauti na misimamo yenu”? Alihoji Kamanda Massawe huku viongozi hao wakiangua kicheko walipokuwa kwenye mpaka huo

mwisho

Maoni