DC Kiteto wananchi ambao hawakuridhika waende mahakamani


                                       Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, (DC) Tumaini Magessa..
                            mwisho Moringe Lemomo, mmoja wa wafugaji Kiteto,akifafanua jambo..

       Mkulima wa kijiji cha Chekanao,Kiteto jina lake halikufahamika mapema akifafanua jambo..

 MKUU wa wilaya ya Kiteto, mkoani Manyara, Tumaini Magessa, amewataka
wananchi wilayani humo, kufungua kesi mahakamani kuthibitisha mauaji
ya watu 30 yalivyojitokeza miaka mitatu iliyopita wakiwa shambani ili hatua

zichukuliwe

Akijibu swali la mwananchi, mjini Kibaya, alisema, mahakama imeshindwa kuwatia hatiani watuhumiwa wa mauaji ya zaidi ya watu 30 waliopoteza maisha kwa kukosa ushahidi

Awali Mbwana Juma (mwananchi) alitaka kujua kauli ya Serikali kuwa ni
watu wangapi waliotiwa hatiani kufuatia mauaji ya watu 30 waliokuwa
wakigombea ardhi miaka mitatu iliyopita, huku kukiwa na hofu tena ya
kuibuka,mauaji mengine.

"Habari nilizonazo, kesi ya mauaji ilitolewa hukumu, hakuna aliyekutwa
na hatia kufuatia mauaji hayo, ila mnaweza kwenda kufungua kesi upya
kama mnaushahidi kuthibitisha bila shaka jinsi mauaji hayo
yalivyojitokeza ili mahakama iweze kutenda haki

Hatua hiyo imefikiwa na wananchi hao, kufuatia vitisho vinavyotolewa
na jamii ya kifugaji (wamasai) kuwa hawako tayari kuona wakulima
katika maeneo yenye mgogoro wa ardhi wakifanya shughuli za kilimo

Akithibitisha hayo Bakari Maunganya mwenyekiti wa wakulima na wafugaji
alisema, chombo kimoja cha habari baadhi ya wafugaji wakitoa matamko
kuwa hawako tayari kuona wakulima wa maeneo ya ndirango kijiji cha
Partimbo wakilima kwa kuwa ni hifafhi

Katika matamko hayo walisema kama panaldol imeshindikana watatumia
paresatam nayo ikishindikana watatumia penv nayo ikishindikana
wataingia kwenye mapigano

Amesema matamko kama hayo yalileta madhara miaka,mitatu iliyopita bila
kukemewa na uongozi kisha watu zaidi ya 30 kupoteza maisha wakati
wakigombea ardhi wakulima na wafugaji ambapo yameanza kurejelewa

"Tunaiomba Serikali yetu iwe na utamaduni wa kushuhulikia matatizo
haraka hasa yanapojitokeza matamko hatarishi kama hayo kwani kuchelewa
kuchukua hatua kunaweza tena kusababisha mauaji"

Mgogoro wa ardhi Kiteto bado unafukuta, huku ikidaiwa kuwepo kwa
jitidada za kukabiliana nao ambapo baadhi ya wananchi wamependekeza
kuwa ili iweze kumalizika Kiteti iwe kanda maalumu ya Kipolisi ili
kuzuia mauaji ya holela

Mwisho

Maoni