DC Simanjiro ataka wachochezi wa migogoro ya ardhi Kiteto kutubu





Picha hapo chini Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Mkoani Manyara (DC) mhandisi Zephania Andriano Chaula akitoa maelekezo ya Serikali kuhusu mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na iliyodaiwa hifadhi ya kijiji cha Partimbo Kiteto Manyara



Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Mkoani Manyara (DC) mhandisi Zephania Andriano Chaula,akimsikiliza Paulo Tunyoni diwani wa kata ya Partimbo muda mfupi baada ya kumalizika kikao cha wananchi wa kitongoji cha Njaniodo kiteto..


 Kaimu katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto,Michael Masinde akifafanua jambo kwenye kikao cha wananchi wa kitongoji cha Njaniodo kijiji cha Partimbo Kiteto Manyara.
HABARI


Akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Njaniodo, kata ya Partimbo wilayani hapo, Mhandisi Chaula ambaye pia ni kaimu mkuu wa Wilaya ya Kiteto amesema, uchochezi unavyoendelea wilayani humo, utaleta madhara kwa wananchi akisema Serikali ya awamu ya tano haitolifumbia macho

“Nimekuja kuhakiki kilichofanyika Nov. 28 mwaka huu, nimeona ni kweli.., kwahiyo walichofanya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya wako sahihi.., nimeona mabango yenu yanasema hamna mgogoro kati ya wakulima na wafugaji, hakuna kitu kizuri hapa duniani kama kuwa pamoja”alisema DC Chaula

Alisema amegundua kuwa mgogoro uliopo ni kati ya wananchi na hifadhi inayodaiwa kuanzishwa na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Partimbo bila kuwashirkisha wananchi na kutaka kuwato watu 1561 wa kitongoji cha Njaniodo, waliokuwa wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji 

Aliwataka wananchi hao kuendelea na shughuli zao akidai ili eneo liwe hifadhi kuna mchakato…nasema kwa viongozi wenye akili nzuri ni lazima wafuate huo mchakato na kwa wale bora viongozi, huwa wanakatisha, mtu yoyote anayekatisha hatakiwi hata kwenye jamii kwasababu ndio mchochezo mkubwa


Halmashauri ya kijiji haina mamlaka ya kujiamulia watakavyo, kama walivyofanya hawa, matatizo mengi ya wananchi hasa wakulima na wafugaji yanatokana na kutofuatwa sheria na taratibu za nchi hii, usiposhirikisha wananchi katika mpango hautafanikiwa na badala yake utaleta madhara


Miongoni mwa kero za wananchi alizotaja ni pamoja na  kuwekewa mabango ya hifadhi ya msitu katika maeneo yao ya kilimo na kubadikwa tangazo la kuondoka ndani ya siku saba, akidai amefuta, viongozi wa kijiji kutokuwa watiifu, waadilifu, na wakweli katika kushughulikia kero za wananchi, wananchi kutoshirikishwa katika mpango wa matumizi bora ya ardh
 

Alisema kwa Wilaya ya Simanjiro, viongozi kama hao huwa  wanachukuliwa hatua mara moja kwa kuswekwa ndani ili hatua za kisheria zifuate mkondo wake, ambapo hata Wilaya ya Kiteto hatua kama hizo zinatakiwa kuchukuliwa mara moja ili kuondoa adha hiyo inayowakumba wananchi kwa maslahi ya watu wachache
 

Hata hivyo akitoa maagizo ya Serikali Mhandisi Chaula, aliwataka viongozi wa Kijiji cha Partimbo kuweka mpango wa matumizi bora ya ardhi na shirikishi, sambamba na wataalamu wa ardhi kupitia mpango huo, kubainisha maeneo yenye mgogoro na kuyatafutia ufumbuzi

Kuhusu suala la viongozi wa kijiji cha Partimbo kwenda kwa mkuu wa mkoa Manyara kulalamika, juu ya maamuzi ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kiteto, kuwarejesha wakulima na wafugaji kuendelea na shughuli zao, alisema makundi hao wanapaswa kuendelea na shughuli na kuahidi hatua za kiutumishi dhidi ya wajumbe hao zitachukuliwa

Kwa upande wake kaimu katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto Michael Masinda, alimhakikishia  mkuu huyo wa Wilaya kuwa maamuzi yaliyofikiwa yalikuwa sahihi, tatizo lililopo ni baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Partimbo kufanya maamuzi bila kushirikisha jamii jambo ambalo limeleta madhara

“Mhe Mkuu wa Wilaya hapa katika maamuzi ya kamati ya ulinzi na usalama, tumehusishwa na rushwa kutoka kwa wananchi, na waliosema ni hao waliokuja huko mkoani, bila shaka umejionea mwenyewe kauli za wananchi wakikuhakikishia yaliyofanyika, sisi viongozi wa Seriikali tutaendelea kutenda haki hata kama tutalaumiwa na watu wasioitakia mema Kiteto”


Akizungumza na Mkuu huyo wa Wilaya Diwani wa Kata ya Partimbo Paulo Tunyoni, alimhakikishia Mkuu huyo wa Wilaya kuwa alikuwa na nia njema kutaka kuhifadhi mazingira na kuahidi kuwa atasimamia mpango wa matumizi kama alivyoelekezwa na Uongozi

mwisho

Maoni