DED Kiteto awashukia wakuu wa idara.



MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Tamimu Kambona, ameapa hatowavumilia watumishi  wa Serikali wilayani humo, watakaoshindwa kuendana na kasi ya Rais DR. John Pombe Magufuli kwa kutowatumikia wananchi.


Akizungumza kwa hisia kali kwenye ukaguzi wa miradi ya ujenzi na umwagiliaji yenye thamani ya zaidi ya mil 400 jana Kambona alisema, baadhi ya wakuu wa idara wamekuwa tatizo akidai, ataanza na Afisa kilimo wa wailaya ambaye ameshindwa kuwajibika na kusababisha manunguniko kwa wananchi.


“Watu kama hawa hatuna sababu ya kuwa nao humu, tumesema kila mtumishi awafikie wananchi walipo, sasa huyu toka tumefika na naibu waziri wa kilimo na umwagiliaji, Mhandisi Izaki Kamwelwe, kuzidua mradi huo zaidi ya mwezi hajafika kuona kinachoendelea”alisema Kambona.


Kwa mujibu wa Kambona, mradi huo wa umwagiliaji Kijiji cha Orgira umegharimu zaidi ya tsh mil 160, pamoja na matumizi ya maji nyumbani, matokeo yake toka uzinduliwe na kuonyeshwa mabomba na jinsi shughuli itakavyofanyika, hakuna kilichoendelea angalia hata wewe mwandishi..alisema Kamboa


“Kwa hili siko tayari kuvumilia, nitafanya kazi na wale ambao tutaendana katika kuwatumikia wananchi, lakini wale watakaoona hawana sababu ya kuwatumikia wananchi, waondoke kama sio kuandika barua wenyewe ya kuacha kazi”alisema huku akionekana kukerwa.


Kutokana na ukaguzi wa miradi hiyo, mkurugenzi huyo amelazimika kuweka kambi katika vijiji vya Sunya na Kijungu ili  kusimamia miradi iliyotakiwa kukamilika toka mwaka jana na ambayo sasa wananchi wamekata tamaa na kuilaumu Serikali kwa kushindwa kuikamilisha .


Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na madarasa manne na vyoo katika shule ya sekondari Kijungi, madarasa mawili, vyoo, na nyumba yenye uwezo wa kuishi familia sita za walimu katika kijiji cha Sunya ya thamani ya zaidi ya mil 400.


Kwa upande wake Ibrahimu mdugi, afisa mtendaji wa kijiji cha Kijungu kuhusu usimamizi huo alisema, utasaidia kukamilisha miradi hiyo kutokana na wahusika kutokuwa karibu nayo hivyo njia pekee ni kuonyesha mfano kama afanyavyo mkurugenzi


“Tungekuwa na kiongozi kama huyu toka awali hii miradi ingeshakamilika, lakini wahusika katika miradi hiyo ambao ni wakuu wa idara, wameshindwa kufika lakini kila mara kama ulivyosikia mkurugenzi akisema hapa kuwa wamekuwa wakimpa taarifa za uongo”alisema Mdugi


Kuhusu majengo hayo alisema awali wanafunzi walikuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa, pamoja na matundu ya vyoo akisema kukamilika kwa miradi hiyo kutaondoa adha kwa wanafunzi na waalimu katika sekta ya elimu


Naye Mwenyekiti wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto Lairumbe Mollel, akizungumzia hali ya miradi wilayani humo alisema, Halmashauri imetenga fedha kwaajili ya miradi viporo ambayo haikumalizika kutokana na sababu mbalimbali zikiwepo uzembe wa wakuu wa idara


Mwisho


Maoni