Michango ya mashirika ya elimu, itambuliwe na Serikali

Rodrick Kidenya, afisa vijana wa Idara ya maendeleo ya jamii Kiteto,akimwakilisha Mkurugenzi mtendaji katika maadhimisho ya miaka kumi toka kuanzishwa huduma ya mtoto chini ya ufadhili wa Compasion Internation Tanzania
anafunzi toka kaya maskini wanaofadhiliwa na Compation Internation Tanzania chini ya mashirika weza ya kidini makanisa Kiteto..

KAZI ya Serikali ni kusogeza huduma za jamaii karibu na wananchi, kwa msingi huo wananchi watanufaika na huduma hizo hasa pale wanapopata huduma kwa wakati na kiwango stahili.

Katika kuhakikisha huduma hizo zinapatikana, mashirika ya umma nayo yamekuwa bega kwa bega na serikali kutimiza lengo lake, huku wananchi wakiendelea kunufaika na huduma za jamii kama vile elimu, afya, maji pamoja na miundombinu.

Katika hatua hiyo baadhi ya maeneo hapa nchini yamekuwa na changamoto katika uekelezaji wa miradi hiyo na kusababisha manong’ono kwa jamii hali inayowafanya wakose imani na Serikali yao.

Hatua hiyo imesukuma makanisa yenye ushirika wenza na Comassion Internation Tanzania klasta ya Kiteto, kutoa msaada wa elimu kwa watoto wanaotoka kaya maskini toka mwaka 2006 ambapo sasa wamewafikia idadi ya wanafunzi 1250.

Toka mashirika hayo yaanze kutoa msaada hiyo, wametimiza miaka kumi Wilayani Kiteto, na kunufaisha wanafunzi wengi kama lilivyo agizo la Serikali kutaka kila mtu aweze kujiendeleza kielimu kama njia ya kujikwamua na umaskini.

Akizungunza kwenye maadhimisho ya miaka kumi, Samwel Maphie, mmoja wa waratibu wa kusaidia watoto hao ambaye pia ni mwalimu, aliwataja wadau wa huduma hiyo kuwa ni kanisa la T.A. G Hermon Kibaya, Anglikan KCC, Anglikan  St Philips, K.K.K. T Kibaya na F.P.C.T Kibaya.

Alisema lengo la wadau hao ni kumkomboa mtoto kutoka kaya maskini kujikwamua kwa kumpatia elimu, huduma ya afya, pamoja na mavazi na hata malazi kwa kuwajengea nyumba ili kumfanya mtoto aweze kusoma na kujisikia kama watoto wengine wenye fursa nzuri ya kusoma.

Huduma hiyo imejikita katika maeneo makuu manne ambayo ni kimwili (Physical Development) Kiroho ( Spiritual Development) Kiakili ( Cognitive) na kijamii ( Social- Emotional Development  ili kumfanya mtoto aweze kumudu mazingira yake

Watoto hao wanagharamiwa matibabu, elimu ya dini, kumfanya mtoto apate nyenzo bora katika kufikia maendeleo yake ya baadaye, pamoja na kumkuza kimaadili ya Kitanzania kuepuka kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya na ulevi.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi, ambaye alikuwa kaimu mkurugenzi wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto, mmoja wa wanafunzi hao, Paulina Jonas Mmbaga, alitaja gharama zinazotolewa katika kumsaidia mtoto huyo kuwa ni pamoja na sare za shule, madaftari, na michango ya maendeleo ya shule.

Pia alisema viwango vya elimu na idadi ya wanafunzi wanaogharamiwa na wadau hao kuwa ni shule za awali wanafunzi (76), shule za msingi (624), Sekondari (545) na elimu ya ufundi wanafunzi (45).

Mbali na huduma hiyo pia alisema, miradi ya kilimo cha kisasa  na ufugaji wa nyuki imeanzishwa ambapo jumla ya mizinga 120 ya nyuki imetundikwa kwaajili ya kupata asali kwa maendeleo ya vituo pamoja na kuanzishwa vikundi vya wazazi vya watoto waliofadhiliwa.

Baadhi ya changamoto zilizotajwa ni pamoja na watoto kuacha shule kabla ya kufikiwa muda wa kuondolewa na program ya ufadhili, mimba za utotoni, kukosa ushirikiano wa kutosha ngazi ya serikali za mitaa, na ushirikiano mdogo kwa jamii.

Zingine ni ukosefu wa madawa hospitali ya umma ambayo husababisha vituo kutumia gharama kubwa kununua madawa nje ya gharama za bima na kukosa ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini wanapokuwa kwenye maadhimisho ya watoto kama vile siku ya mtoto wa Afrika

Kwa upande wa mgeni rasmi Rodrick Kidenya kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto akizungumza na mamia ya wanafunzi hao pamoja na wazazi aliwapongeza kwa kufanya maadhimisho ya miaka kumi toka kuanzishwa huduma hiyo,alisema Serikali inatambua kazi za mashirika

Alisema Serikali haiwezi kukuwa nyuma ili hali kazi zinazofanyea na mashirika zinakuwa na tija, na kuwasihi viongozi hao kuendelea na moyo wao huo wa kuisaidia Serikali pamoja na kuendelea kuwajulisha kinachoendelea ili waweze kushirikiana katika kumhudumia mtoto.

“Niwaombe tu…msikate tama kwa kuona kuwa Serikali imewatelekeza, tumekuwa nanyi pamoja katika kuhudumia jamii na tunatambua mchango wenu, ila msisite kuendelea kutusaidia pamoja na kupeana taarifa”alisema mkurugeni huyo wa Halmashauri.

Naye Mchungaji Petro Lohay  wa FPCT Kiteto, aliwataka jamii kutumia fursa iliyopo kupitia mashirika hayo kuwapa watoto wao elimu na kuachana na tabia za kuwakatisha masomo kwa kuwaozesha ama kuwatuma kwenda kuchunga mifugo

“Tumeshuhudia wanafunzi wengi wakikatishwa masomo kwa sababu mbalimbali, hata Serikali imekiri kuwa hili ni tatizo kuna wanafunzi wenenu 97 wameacha shule kwa kupachikwa mimba, hili halivumiliki tuamke na kupinga tabia hii, tunaomba serikali isaidie kukabiliana na tatizo hilo”alisema

Nao baadhi ya wanafunzi hao wakiwasilisha ujumbe kwa nyia mbalimbali zikiwemo ngonjera na nyimbo waliwataka wazazi kubadilisha na kuendana na mfumo wa sasa katika kumhudumia mtoto kupata malezi bora ili aje kuwa mtanzania mwema na mwenye tija kwa Taifa lake.

Mwisho.

Maoni