Ikulu ya Tanzania
UTAWALA wa Rais, John Pombe Magufuli, umeendelea kukonga nyoyo za
watanzaia ambapo, Bendera Maguluko (55) wa Kiteto mkoani Manyara,
ameapa kwenda Ikulu kumpa Rais zawadi ya bata dume.
Akizungumza kwa hisia kali Maguluko alisema, katika kuunga mkono
jitihada za Rais Magufuli, ameamua kutafuta nauli ya kwenda kumpa
zawadi ya bata dume aliloandaa, kama shukrani na ishara ya kuunga
mkono jitihada za kupambana na mafisadi nchini
“Kuna kila sababu ya watanzania kutambua mchango wa Rais
Magufuli..binafsi natoa shukrani za dhati kwa Mungu, kwani kazi
anayofanya kwa watanzania ni kubwa na inapaswa kuungwa mkoni na watu
wenye nia njema” alisema huku akiwa na hali ya kuguswa na utawala wa
JPM
Baadhi ya kazi zilizomsukuma amshukuru Rais Magufuli ni pamoja na
kukabiliana na watumishi hewa, wanafunzi hewa, kufanikisha zoezi la
Serikali kuhamia Dodoma, ununuzi wa ndege sita, kufuta baadhi ya
sherehe zilizowagharimu wananchi, pamoja na maboresho ya elimu, afya,
maji na miundombinu
Kwa upande wake Maulidi Kijongo (58) mwananchi alisema, viongozi wa
Serikali ngazi mbalimbali wasiendelee kumshangaa Rais Mgufuli kwa kazi
anayofanya badala yake kila mtu awajibike katika nafasi yake, ili
wananchi waweze kunufaika na utawala huo
Alisema kila kona ya nchi ya Tanzania wananchi wengi wamekuwa
wakimsubiri Rais Magufuli kutatua matatizo yao, kana kwamba hakuna
viongozi katika maeneo hayo, na kuwataka viongozi hao kuacha kusubiri
kuja kufukuzwa kazi katika maeneo yao
“Kila kiongozi angefanya kazi kama Rais Magufuli.. wananchi tungekuwa
na neema katika nchi yetu, lakini imekuwa kinyume chake na kujikuta
tukipoteza maisha kutokana na baadhi ya viongozi kushindwa kuwajibika
na kusababisha watu kuuana (wakulima na wafugaji)
Watanzania tuwe na utamaduni wa kushukuru japo kuwapa moyo viongozi
wetu, kwani kutofanya hivyo inawakatisha tama na kujiona kuwa hawana
tija katika kazi wazifanyazo, hivyo kila mtu kwa nafasi yake anapoona
kuna jambo la kuunga mkono ama kukosoa afanye hivyo,alisema Ramadhani
Konki (mwananchi)
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni