Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa
ZIARA ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, anayekusudiwa kuwasili hivi
karibuni Wilayani Kiteto mkoani Manyara,imeanza kuleta hisia tofauti
kwa wananchi huku baadhi ya viongozi wakihofia ajira zao kuyeyuka.
Hofu hizo zimetokana na mfumo wa utawala wa Serikali ya awamu ya tano,
ambayo umma umeshuhudia baadhi ya viongozi wakiwajibishwa kutokana na
kutowajibika,uzembe kazini,utoro pamoja na matumizi mabaya ya
madaraka.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi
wamesema,wanakusudia kusikia kauli ya Serikali juu ya migogoro ya
ardhi ya muda mrefu ambayo imesababisha zaidi ya wakulima na wafugaji
30 kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.
Wamesema kwa sasa hakuna jibu sahihi toka kwa viongozi wa Kiteto juu
ya wangapi walichukuliwa hatua kufuatia mauaji hayo yaliyojitokeza
huku wananchi wakiendelea kunung'unika
"Ninachojua mtu akifa kuna uchunguzi wa mamlaka husika, na wahusika
kufikishwa mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake, nashanga kwa
Kiteto maafa hayo yametokea zaidi ya watu 30 lakini hakuna
aliyechukuliwa hatua"alisema Bakari Maunganya mkulima.
Alisema ujio wa Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa, Wilayani Kiteto,
unakusudiwa kutoa majibu ya maswali hayo ambayo yamekosa majibu kwa
muda mrefu, huku wananchi wakidaiwa kusubiria majibu hayo kwa muda
mrefu.
Kwa upande wa baadhi ya viongozi wa Serikali ambao hawakutaka kutaja
majina yao walisema, ziara hiyo inaweza kuleta madhara kwa baadhi ya
viongozi haswa wale waliohamishwa kutokana na sababu mbalimbali
zikiwemo kusababisha migogoro ya ardhi
"Viongozi wengi Sana wa kada mbalimbali wamehamishwa kutokana na hii
migogoro, Waziri Mkuu akija atayabaini na huenda akaagiza waje
kujieleza kutokana na tuhuma zao"alisema mmoja wa watumishi wa
Serikali Kiteto ambaye hakutaja kutajwa majina
Kwa mujibu wa Katibu tawala wa Wilaya ya Kiteto, Ndaki Stephano,
alikiri kuwepo mwa ujio Waziri Mkuu akidai ni mapema kuzumgumziwa
ingawa ziara hiyo ni yakawaida.
Alisema wilaya ya Kiteto ina changamoto ya migogoro ya ardhi ambazo kwa
kiasi kikubwa zimedhibitiwa, akidai toka utawala ubadilishwe karibia
ngozi zote hakuna maafa yaliyojitokeza kwa miaka miwili tofauti na
kipindi kilichopita.
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni