Ramani ya mpaka wa wilaya ya Kiteto na Kilindi, ambayo alama nyekundu inaonyesha mpaka wa mwaka 1961 GN namba 65 ambayo Serikali imetaka uheshimiwe na pande hizo..
Katibu Tawala mkoa wa Manyara, Eliakimu Maswi akimwonyesha ramani Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa ya mpaka wa wilaya ya Kiteto iliyopo Manyara na Kilindi ya Tanga..
waziri Mkuu Kassimu Mjaliwa akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Tanga mpakani mwa Kiteto na Kilindi..kushoto ni mkuu wa mkoa wa Manyara, Dr. Joel Nkaya Bendera wa manyara,..
Wananchi wakimkaribisha kwa mabango Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa..
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akionyesha moja ya mabango aliyoandikiwa kuwasilisha ujumbe..
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa, kushoto akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian wakifuatilia hutuba ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa.
Wajumbwa wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kilindi wakifuatilia hutuba ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa...
Wajumbwa wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kiteto wakifuatilia hutuba ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa...
Waandishi wa habari wakiwa katika majukumu yao..
Waandishi wa habari wakiwa katika majukumu yao..
Tumaini Kambona Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kiteto, akipeana mkono na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa..
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa, akipeana mkono na Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa..
Kamati ya ulizi na usalama kiteto wakimpa heshima Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa..
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dr Joel Nkaya Bendera akisisitiza jambo..
Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian akitoa salamu kwa wananchi wa Kiteto na Kilindi..
Waziri wa ardhi Nyumba na makazi, Williamu Lukuvi akisisitiza jambo..
Waziri wa Serikali za mitaa Tamisemi, Geoge Simbachawene akisisitiza jambo..
NA. MOHAMED HAMAD
WAZIRI mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassimu Majaliwa,
amewataka wananchi kuheshimu mipaka ya kiutawala , na kuacha kuhamisha
alama ili kuepuka migogoro inayojitokeza hapa nchini.
Akizungumza mpakani mwa wilaya ya Kiteto iliyopo mkoani Manyara na
Kilindi iliyopo mkoani Tanga, Majaliwa amesema, mipaka imelenga
kusaidia watawala kuongoza nchi, hivyo kitendo cha wananchi kupigania
mipaka hakina tija.
Alisema Serikali inatambua mpaka wa Kiteto na Kilindi wa mwaka 1961
wenye GN namba 65, akisisitiza hautabadilika bali watauboresha kwa
kutafsiri kwa wananchi ili waweze kuelewa huku akiwaonya baadhi ya
watumishi wa Serikali kutumia migogoro kwa kujinufaisha .
Aliwataka wakuu wa mikoa ya Manyara na Tanga, kuhakikisha kuwa
wanasimamia amani mpaka Serikali itakapokamilisha zoezi la kuweka
alama upya zilizong’olewa huku akiwataka wakulima na wafugaji
kuendelea na shuguli zao bila kubughudhiwa.
Akiwahakikishia wananchi kuwa mgogoro wa mpaka umeanza kushughulikiwa
kwa kuwaapisha viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za Kiteto
na Kilindi, Wabunge, Wenyeviti wa Halmashauri na madiwani kuhakikisha
wanasimamia agizo hilo la Serikali ili wananchi waishi kwa amani.
Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi Williamu
Lukuvi, alisema kazi ya kuweka alama hizo itaanza mapema wiki ya
kwanza ya mwezi wa pili mwaka huu ili kupunguza madhara ya wananchi
wanayopata katika maeneo yao.
“Mhe Waziri Mkuu naomba niwahakikishie umma wa wananchi hawa kuwa,
zoezi hili nitalifanya mapema kabisa katika wiki la kwanza la mwezi
ujao ili kumaliza mgogoro huu ambao umesababisha madhara makubwa kwa
wananchi” .
Naye Waziri wa Serikali za mitaa Tamisemi, Geoge Simbachawene, alitaka
wananchi kuendelea kuiamini Serikali ya awamu ya tano, kwakuwa ina nia
njema katika kuwatatulia matatizo yao akisisitiza watumishi
watakaobainika kuwa chanzo cha migogoro hiyo hawatakuwa na nafasi
Serikalini.
Awali wananchi wa kijiji cha Mafisa Wilayani Kilindi, waliweka mpaka
wao kwa kutenganisha mkoa wa Tanga na Manyara, kufuatia mgogoro wa
ardhi kati yao na wananchi wa Kijiji cha Lembapuli kilichopo Wilayani
Kiteto na kusababisha madhara .
Kwa mujibu wa Diwani wa kata ya Lolera Kosey Lehinga (Chadema)
,alimweleza Waziri Mkuu kuwa mgogoro huo ulisababisha maafa ya watu
watatu, gari moja aina ya Noah kuchomwa moto na mashine ya maji
kuharibiwa kwa kuteketezwa kwa moto katika kijiji cha Lembapuli.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kiteto Emmanue Papian (CCM)
aliwahakikishia wananchi wa Wilaya ya Kiteto na Kilindi kuwa watafuata
maagizo ya Serikali ambayo yametolewa na Waziri Mkuu, akisema
maelekezo hayo ni ufumbuzi wa mgogoro kati ya Wilaya hizo.
Naye Omari Kigua Mbunge wa Jimbo ala Kilindi (CCM) aliwataka wananchi
hao kuwa na subra akisisitiza kuwa anamwamini Waziri Mkuu Kassimu
Majaliwa na Timu nzima ya utawala wa awamu ya tano akisema ujio wake
katika eneo hilo anamatumaini akisisitiza kila mtu awajibike katika
nafasi yake.
Kwa upande wa Baadhi ya wananchi wa kilindi na Kiteto walisema,
maelekezo hayo yatakuwa suluhisho la mgogoro wa ardhi endapo baadhi ya
viongozi wa Serikali hawatatumia migogoro kama vyanzo vyao vya mapato.
“Tumekuwa na tatizo hapa wataalamu wetu wa ardhi, wanakuwa na
maelekezo tofauti kila kukicha, leo wanaweza kukuonyesha mpaka hapa
kesho pale, sasa tunaoumia ni wananchi kwa kushindwa kujua kuwa tuko
wapi kiutawala” alisema Bakari Issa Mwananchi wa Kilindi.
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni