Wanawake Kiteto watishia kufunga uzazi

Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Emmanuel Papian akiwa katika mkutano wa kushukuru wananchi kwa kumuamini kuongoza Jimbo Hilo..
wananchi wa mji wa Kibaya katika mkutano na mbune wao..
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa akiwa katika mkutano na wananchi wa Kibaya..

Na, MOHAMED HAMAD


KAULI za kejeli, matusi na vipigo kwa wajawazito, wilayani Kiteto
mkoani Manyara, zimetajwa kuwa tishio kwa wanawake kutata kufunga
uzazi mpaka wahakikishiwe kutatuliwa kero hiyo, ili waendelee na
uzazi.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wezake Farida Omari mkazi wa Kibaya
alisema, lalamiko hilo limekuwa la kujirudia kila mara anapowasili
kiongozi wilayani humo bila ufumbuzi na kuiomba Serikali kuchukua
hatua.

Ameeleza hayo mbele ya mbunge wa Jimbo la Kiteto Emmanuel Papian (CCM)
alisema, hawawezi kiuendelea na uzazi mpaka ahakikishiwe usalama wao
kwa kutatuliwa kero hiyo ambayo imedaiwa kuchukua muda mrefu bila
ufumbuzi.

“Mama mjamzito akienda hospitali ya Kiteto sehemu ya kujifungulia,
mambo anayokutana nayo ni makubwa utadhani yuko na FFU, hili
halivumiliki Mhe. Mbunge tunaomba kero hii ishe kwani kuendelea kwake
kutaleta madhara makubwa”alisema Farida Omari (mwananchi).

Alisema mbali na matusi, kejeli, vipigo wakati wa kujifungua, baadhi
yao wamekuwa wakitelekezwa kwa kutopata msaada wa kujifungua na
kujikuta wakijifungua wenyewe bila kupata usaidizi kwa madai ya
kutofika na vifaa, gloves.

Akionyesha kukerwa na hali hiyo, Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Emmanuel
Papian (CCM) alimtaka Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
kuchukua hatua dhidi ya watumishi hao wanaolalamikiwa akidai hilo
halivumiliki, huku akisema baada ya hao kuna waungu watu ambao ni
wenyeviti wa vijiji na watendaji wao.

“ Ndugu yangu Kambona, unataka ushahidi gani..hili halitoshi kuchukua
hatua? nakumbuka haya malalamiko ni ya muda mrefu sana yamekuwa
yakujirudia katika hospitali hii..amka sasa timiza wajibu wako kwani
kutofanya hivyo ni hatari ambayo itatugharimu baadaye”.

Alisema kama mwakilishi wa wananchi hatokuwa tayari kuona wananchi
wakinyanyasika wanapohitaji huduma za jamii, akidai mtumishi wa umma
asiyeendana na kasi ya Rais John Magufuli hatovumilika.

Akiwa katika mkutano huo mkurugenzi mtendaji wa halamsauri ya wilaya
ya Kiteto, Tamimu Kambona, aliwataka akinamama hao kuendelea na uzazi
akisema, ameshamwandikia barua ya kumshusha cheo muuguzi huyo Dr.
Samsom nyakibali, ambaye ameshindwa kuitendea haki nafasi yake.

“Endeleeni na mambo ya uzazi..akinamama nimeshamwandikia barua huyu
bwana, amelalamikiwa sana kwa kushindwa kuwajibika katika nafasi yake,
na kuhusu kauli chafu kejeli, natua wito wangu kwa watumishi wote wa
hospitali ya Kiteto waache mara moja wawajibike nitawafikia
nao”alisema Kambona

Kuhusu uhaba wa madawa katika hospitali hiyo ambyo nayo yalilalamikiwa
kwa wagonjwa kulazimishwa kwenda kununua dawa katika maduka ya wati
binafsi, Kambona alisema wanampaka wa kuanzisha duka la Serikali
kupunguza kero hiyo akisema alihakikishiwa na Waziri Mkuu Kassimu
Majaliwa kuwa dawa zitaletwa kwa wingi.

Mwisho

Maoni