Diwani Kiteto, mbaroni kwa rushwa ya laki 5

Picha ya Madiwani Kiteto wakiwa kwenye kikao cha Halamshauri ya Wilaya..


Na, MOHAMED HAMAD,
DIWANI wa kata ya Ndirigish, Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, Chitu Daima (CCM), anashikiliwa na kikosi cha kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU kwa tuhuma za kudai na kupokea rushwa ya shilingi laki tano.

Tukio hilo limetokea Kijijini hapo kufuatia wananchi kumtuhumu diwani huyo kupokea rushwa jambo lililowagharimu fedha nyingi ndipo wakaamua  kutega mtego na kufanikiwa kumnasa akipokea kutoka kwa mmoja wa wananchi.

Kwa mujibu wa Ainoti Sepewa mmoja wa wafugaji aliyedaiwa fedha hiyo ili aweze kupatiwa maeneo ya kulisha mifugo yao alisem,  awali walimpa diwani huyo zaidi ya mil moja bila mafanikio ya kupata maeneo kwaajili ya shughuli za ufugaji.

“Baada ya kuchoshwa na hali hii, nililazimika kwenda PCCB kuomba msaada zaidi, ndipo akataka nimpe laki tano nikamwahidi kuwa naenda mnadani kuuza ng’ombe na kufanikiwa kupewa fedha na PCCB na kumkamatisha”alisema mwananchi huyo.

Alisema awali wananchi kwa pamoja walikubaliana kumega sehemu ya hifadhi yao ya Emboley Murtangos, ili wagawane wakulima na wafugaji, badala yake eneo hilo limegawiwa wakulima peke yao na kusababisha manug’uniko makubwa.

Kwa upande wake Mathew Isaya, alitaja baadhi ya madhara waliyopata kutokana na rushwa hizo kuwa ni pamoja na kutopatikana haki na kusababisha mahusiano mabaya kati ya wakulima na wafugaji kupigana.

Naye Kadege Mario (mwananchi) wa Kitongoji cha Kuti, kijiji cha Ndirigishi alisema, mara ya kwanza walimpa laki tano, laki tatu, siku nyingine walimpa laki nne na mbuzi mnyama, akisema maisha yao ni duni kufuatia kuhonga viongozi.

Akizungumzia migogoro hiyo Daniel Lucas (mwananchi) Wilayani Kiteto alisema, baadhi ya viongozi wamekuwa tatizo kwa jamii nakuomba Serikali kuingilia kati huku akiwataka wakulima na wafugaji kuwa na subra inapojitokeza migogoro

Kwa upande wake Jastine Maingu, Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya Kiteto amekiri kutokea tukio hilo akisema, hawezi kuzungumza chochote kwakuwa wako katika hatua ya awali pamoja na kufanya mahojiano juu ya tukio hilo ambapo hadi sasa mtuhumiwa anashikiliwa kwa tukio hilo

Nao baadhi ya madiwani akiwemo Mussa Britoni (CCM) kata ya Sunya alisema vyombo vya sheria vitende haki juu ya tukio hilo. huku diwani Zamzam Ramadhani (Chadema) alisema madiwani wasijihusishe na rushwa kwa sababu ni adui wa maendeleo

Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Tumaini Mgessa, aliwasihi viongozi wa Serikali pamoja na Siasa kutojihusisha na rushwa kwakuwa imekuwa ikipoteza haki za wananchi pamoja na kuchangia migogoro ya ardhi kati ya weakulima na wafugaji.

“ Serikali ya awamu ya tano, tutahakikisha tunapapamba na na rushwa ili kuwafanya wananchi wajivunua Serikali yetu, na kamwe hatutamwonea haya mtu yoyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa” alisema (DC) Magessa huku akionekana kuchukizwa na tabia hiyo.

Mwisho

Maoni