Askofu Isaya Chamballa wa kanisa la Anglikan akiomba dua ya maridhiano ya wakulima na wafugaji Kiteto...
Padri wa Kanisa la RC Kiteto akiomba dua ya maridhiano ya wakulima na wafugaji Kiteto..
Kiongozi wa mila wa jamii ya kifugaji Mbambire Oleikurukuru akiomba dua ya maridhiano ya wakulima na wafugaji Kiteto...
Mwenyekiti wa wenyeviti wa mila Abubakari Mrisho akiwa katika dua la maridhiano ya wakulima na wafugaji Kiteto..
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dr. Joel Nkaya Bendera akifafanua jambo ziara ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa..
Waziri Mkuu Kassimu Kassimu Majaliwa akishiriki dua ya pamoja kuombea wakulima na wafugaji Kiteto..
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa akishiriki dua ya pamoja ya wakulima na wafugaji kuombea amani...
Waziri Mkuu Kassimu Kassimu Majaliwa akiwa Kiteto..
Waziri Mkuu Kassimu Kassimu Majaliwa akiwa Kiteto Kiteto..
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dr. Joel Nkaya Bendera..
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dr. Joel Nkaya Bendera akimkabidhi taarifa ya Mkoa Waziri Mkuu Kassimu kassimu Majaliwa Wilayani Kiteto..
Mbunge Viti maalum Marther Jaki Umbulla katikati, Emmanuel Papian kushoto wakifuatilia jambo ziara ya Waziri Mkuu Kiteto..
Afisa upelelezi wilaya Bw. Malema kushoto, mshauri wa mgambo wilaya na Mkuu wa kituo cha Polisi Kiteto Patrick Kimaro (SABASITA) wakifuatilia hutuba ya waziri Mkuu Kassimu Kassimu Majaliwa Kiteto..
Afisa habari wa Mkoa wa Manyara Bi. Remija na Mbwana Jumaa wa TV, Thed Chale wa habari leo Imani wakifuatilia hutuba ya Waziri Mkuu Majaliwa..
Madiwani wa Halmashauri ya Kiteto wakifuatilia hutuba ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa..
Wananchi wa Kiteto wakifuatilia hutuba ya Waziri Mkuu Kassimu Kassimu Majaliwa..
Wananchi wa Kibaya wakiomba Dua ya maridhiano ya Wakulima na Wafugaji Kiteto..
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akiwa kwenye mkutano kiteto..
Mbambire Oleikurukuru Kiongozi wa mila wa Kimasai akionyesha jani ishara ya amani Kiteto mbele ya Waziri Mkuu...
Waziri Mkuu Kassimu Kassimu Majaliwa, akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa ya namna ya kutatua migogoro ya ardhi..
Taratibu za kimila zikifanyika katika kupooza damu iliyomwagika kutokana na mapigano ya wakulima na wafugaji Kiteto..
NA. MOHAMED HAMAD
WAZIRI Mkuu kassimu Majaliwa, amehitimisha migogoro ya ardhi Kiteto kati ya wakulima na wafugaji uliodumu kwa muda mrefu na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu 30 na wengine kujeruhiwa kwa kufanyika dua mbalimbali kutoka kwa viongozi wa dini, mila pamoja na wananchi.
Akizungumza na mamia ya wananchi hao, Waziri Majaliwa alisema mgogoro mingi ya ardhi inachangiwa na baadhi ya viongozi wa vijiji ambayo hata Mkuu wa Wilaya anaweza kushughulikia isipokuwa tatizo ni viongozi hao kutoamua kumaliza matatizo hayo.
Alisema Serikali ya awamu ya tano haiko tayari kuona wananchi wakilalamika na kuwataka wateule wa Serikali wote kutimiza wajibu wao katika kuwahudumia wananchi..
Akifafanua zaidi Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa alisema kwa sasa hataki kusikia wilaya ya Kiteto kuwa na migogoro ya ardhi akisema mipaka inayotambulika ni ya mwaka 1961, na kama wilaya imeamua kugawanywa kuwa wilaya mbili haitaathiri wilaya ya jirani kama ilivyo Kondoa na Chemba, Kiteto na Simanjiro na kwingineko..
Waziri Mkuu alizungunza na watumishi wa Serikali, baadaye alienda kuweka jiwe la msingi jengo la Halmashauri ya Wilaya la thamani ya zaidi ya bil 4, baadaye alishiriki dua ya pamoja kuombea amani ya Kiteto iliyokuwa imetoweka kwa kushirikisha makabila makuu manne, wanguu, wamasai, wakaguru na wagogo
mwisho
Maoni
Chapisha Maoni