Agizo la RC Manyara laanza kutekelezwa Kiteto.



Mkuu wa Wilaya ya Kiteto (DC) Tumaini magessa, akizungumza na mtoto aliyedaiwa kutoandaliwa kielimu katika kijiji cha Kimana kata ya Partimbo Kiteto, Manyara..
 Mkuu wa Wilaya ya Kiteto (DC) Tumaini Magessa akisisitiza jambo.. 
Kamati ya ulinzi na usalama Kiteto..
Wananchi wa Kijiji cha kimana maeneo ya pori namba moja..wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa..
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto (DC) Tumaini Magessa..
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimana Kashura Ngalanya akifafanua jambo..
Wananchi wa Kijiji cha Kimana eneo la pori namba moja..
Baadhi ya wanafunzi katika maeneo ya pori kwa pori waliokosa shule kwa wazazi wao kwenda kujihusisha na kilimo ambako hakuna huduma za jamii...



NA. MOHAMED HAMAD

AGIZO la Mkuu wa mkoa wa Manyara, Dr. Joel Nkaya Bendera,Wilaya ya Kiteto la kuhakiki umiliki wa mashamba yao, limeanza kutekelezwa, sambamba na kutolewa elimu kwa wananchi hao juu ya namna ya kumiliki mashamba hayo.

Akizungumza mbele ya wananchi hao, DC Magessa, alisema idadi kubwa ya wamiliki wa mashamba hayo hawana vibali na kuwataka kwutafuta uhalali wa umiliki huo..

Alisema uhakiki huo utabaini watu wenye kumiliki mashamba makubwa na jinsi walivyoyapata, huku akisisitiza kuwa Serikali ya Kijiji mwisho wa kugawa ardhi ni ekari 50.

Pia aliwataka wananchi wa maeneo ya kisima, pori namba mbili kutoanzisha makazi isivyo halali, akiwataka kambi kuu iwe eneo la pori namba moja liwe kama kitongoji

Kwa mujibu wa taarifa, imeelezwa kuwa, kijiji cha Kimana kina jumla ya watu 15,000, chenye eneo kubwa kuliko vijiji vinginge Wilayani Kiteto..

Mwisho.

Maoni