Taarifa za hali ya hewa ndio suluhisho la matatizo ya wakulima, wafugaji nchini.


                             Dr. Agnes Kijazi, Mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa nchini..
                                                                 Uhaba wa maji..
                                                            Uharibifu wa mazingira...
 


Na, MOHAMED HAMAD.
Kwa muda mrefu, wakulima na wafugaji hapa nchini wamekuwa na changamoto lukuki katika shughuli za kilimo na ufugaji, hali inayofanya wakati mwingine kupoteza maisha kwa kugombea ardhi.

Makundi haya  yamekuwa na uhasama mkubwa, wanapokuwa katika shughuli zao za kila siku, kutokana na mabadiliko ya tabianchi ambapo yamefanya wawe na tabia za kuhamahama katika shughuli hizo.

Katika hatua hiyo madhara makuu manne yamejitokeza kutokana na mabadiliko ya tanianchi ambayo  katika sekta ya kilimo, maji, afya na nishati, hali inayofanya watu waishi kwa taabu huku wakiitaka Serikali na hata mashirika ya umma kuwasaidia.

Eneo la la kilimo mara nyingi wakulima wameshughudia kupungua kwa uzalishaji wa mazao kuongezeka kwa magonjwa na wadudu waharibifu wa mazao, hali iliyosababisha mkulima kukosa mazao na kujikuta wakipata hasara

Kufuatia hali hiyo wakulima wamekuwa na tabia ya kuhamahama, wakiamini kuwa mashamba mapya yatawapatia kipato kikubwa huku wakisafisha mashamba mapya kwa kufyeka misitu.

Wakati wakufyeka misiti na kuchoma majani, husababisha ardhi kuwa wazi hivyo kufanya unyevu kutowena katika uso wa ardhi kutokana na mionzi ya jua na kusababisha jangwa katika eneo husika.

Kupungua kwa mvua ni eneo lingine ambalo inasababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, hali inayoathiri upatikanaji wa maji safi na salama, na kufanya binadamu na mifugo na hata mimea kuishi kwa taabu

Binadamu, mifugo na mimea ikikosa maji hufa, hivyo kila mara kumekuwepo na jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali na mashirika ya umma, katika kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa kadiri iwezekanavyo

Kwa mujibu wa sera ya maji ya Taifa, kila nyumba inatakiwa isikose maji safi na salama kwa umbali usiozidi mita 400, hivyo katika kukabiliana na hilo jitihada kubwa zinapaswa kufanya kupunguza adha hiyo.

Wilaya ya Kiteto ina uwezo wa kujimudu kupata maji safi na salama maeneo ya vijijini kwa 36%, huku katika maeneo ya mijini ikiweza kuhudumia wananchi wake kwa 37%, jambo ambalo limedhoroesha maendeleo ya wananchi toka wilaya izinduliwe mwaka 1974.

Kupungua kwa vina vya maji katika mabwawa yanayozalisha umeme na kuathiri uzalishaji wa umeme ni eneo lingine katika mabadiliko ya tabianchi, hivyo ili kuweza kukabiliana na hali hiyo, kuna kila sababu ya wananchi kupanda miti sambamba na kuacha kufanya shughuli za kilimo mita 60

Kwa mujibu wa taratibu ya uhifadhi wa mazingira wananchi wanashauriwa kutolima kwenye kingo za mito na mabwawa ili kuepuka bwawa kujaa matope, na kusababisha kupasua mara mvua zinaponyesha

Maeneo mengi yaliyochimbwa mabwawa na kuruhusu shughuli za kilimo, wamejikuta wakipata hasara kwa mabwawa hayo kupasua, na kuwaacha wananchi wakilia shida ya maji kwa kukosa maji kutokana na madhara hayo.

Suala la kuongezeka kwa matumizi ya nishati kwa ajili ya viyoyozi kutokana na ongezeka la joto, nalo imekuwa tishio, hali inayofanya wananchi kuishi kwa taabu, hivyo ili kukabiliana na hali hiyo kuna kila sababu ya kufuata maelekezo ya kitaalamu kukabiliana na hali hiyo.

Hata hivyo madhara yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi ni kuongezeka kwa matukio ya magonjwa ya malaria na magonjwa ya mlipuko, hivyo kuligharimu Taifa fedha nyingi kwa kuokoa wananchi wake.

Ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, wakulima na wafugaji hawana budi kutumia taarifa za hali ya hewa, ambazo hutolewa na mamlaka ya hali ya hewa nchini, katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Taarifa za hali ya hewa, kwa kawaida hutoa tahadhari juu ya madhara yanayoweza kujitokeza, hivyo wakulima na wafugaji na hata wadau wengine wa hali ya hewa, wanaweza pia kutumia taarifa hizo kuepuka madhara hayo.

Wakulima wakipata taarifa ya hali ya hewa, ni rahisi kuchukua hatua, kama wataelezwa mvua ni chache wataweza kulima mazao ya muda mfupi, hali kadhalika wafugaji watatakiwa kuishi kulingana na mabadiliko ya tabia nchi yatakavyojitokeza ili wasiweze kuathirika.

Wananchi wilayani Kiteto na maeneo mengi hapa nchini wameshuhudia mimea ya wakulima ikikauka shambani  kwa kukosa mvua, huku mifugo ya wafugaji ikifa kwa kukosa malisho, jambo ambalo wangeweza kutumia taarifa za hali ya hewa wasingekutwa na madhara hayo.

Nashauri ili kuepuka madhara ya mabadiliko ya tabianchi kuna kila sababu ya taarifa za hali ya hewa kuwafikia wadau wa hali ya hewa na kuzitumia ipasavyo kwani kwa kufanya hivyo wataweza kulinda mali zetu

Wakati mwingine hakuna budi kuwashirikisha walaalamu katika shughuli  ili waweze kushauri kitaalamu..mfano mfugaji anaweza kuuza mifugo yake anapopata taarifa kuwa kipindi kijacho kuna tatizo litakaloathiri mifugo yake.

Mwisho.

Maoni