CWT Kiteto, wafundisha walimu ujasiriamali


Viongozi wa chama cha waalimu CWT (ke) wilayani Kiteto, wakifundishwa ujasiria mali..
 Hatua mbalimbali ya masomo ya ujasiria mali kwa (waalimu) wanachama (ke) wa CWT Kiteto (ke)..
 Waalimu, (ke) wanachama wa CWT Kiteto wakiwa katika mafunzo ya ujasiria mali..
 Katibu wa CWT Kiteto Bi. Rosemery Mwakibeth, akitoa maelekezo ya masomo ya ujasiria mali CWT kitengo (ke)...
Baadhi ya bidhaa, zilizotokana na mafunzo kwa waalimu wa CWT (ke) Kiteto ya kutengeneza bidhaa..


NA. MOHAMED HAMAD
KATIKA kuwaimarisha waalimu kiuchumi, chama cha waalimu CWT Wilayani Kiteto, mkoani Manyara, kimetoa mafunzo kwa waalimu wanawake, ili wafanye ujasiriamali baada ya kazi,kuondokana na umaskini wa kipato ndani ya jamii.

Akizungumza na waalimu hao, Mkt wa chama hicho, Paulo Gwacha, aliwaambia mwonekano wa waalimu ndani ya jamii sio mzuri, hali ambayo inaweza kushusha ufanisi wa kazi zao kutokana na umaskini wa kipato unaotokana na kipato kidogo wanachopata kutoka Serikalini..

"Mishahara tunayopata toka Serikalini haiwezi kukidhi haja, ndio maana chama kimeamua kuwajengea uwezo wa kuwa wajasiriamali ili muweze kufanya ujasiriamali muda wa mapumziko baada ya kufanya kazi za Serikali

Alisema walimu wasipojiongeza hasa katika kipindi hiki, kuna uwezekano wa kushuka kwa ufanisi wa kazi zao, kwani kila mara watakuwa wanawaza maisha kuliko kufanya kazi waliyoajiriwa.

Kwa upande wake, Agnece Lyatu, Katibu wa kitengo cha wanawake CWT Kiteto alisema, mafunzo hayo yataleta tija kubwa kwao akisema jumla ya watu 1,500 wakiwemo waalimu watanufaika na mafunzo hayo wilayani Kiteto..

"Hapa tumejifunza namna ya kutengeneza batiki, urembo wa aina mbalimbali, soko lipo tutauza kwa waalimu na hata jamii na kupata fedha ambazo zitatusaidia kukidhi mahitaji yetu na familia, mishahara haitoshi"

Naye Elizabeth Bella (mwalimu) aliomba Serikali kusikia kilio chao cha muda mrefu ambacho hakijatatuliwa, kuhusu likizo, kupanda madaraja,matibabu na uhamisho, akisema kutosikilizwa kunafanya waione Serikali kutowajali

Rosemery Mwakibeth, ni Katibu wa chama cha walimu Kiteto, akizungumza na walimu hao alisema, chama kitaendelea kumkumbusha mwajiri ili aweze kutimiza wajibu wake huku akiwasihi walimu kuendelea na kazi ya kufundisha

"Endeleeni kufundisha chama tunafuatilia mambo yenu..ila onezeni ujasiriamali kama sehemu ya majuku yenu, waalimu msikae kusubiri mshahara, hautoshi ikizingatiwa mnategemewa na familia zenu"

Mafunzo kwa waalimu hao kitengo (ke) yamelenga kuwajengea uwezo ili nao waweze kwenda kufundisha wenzao elimu hiyo kwa lengo la kujikwamua na umaskini wa kipato.

mwisho...

Maoni