Mamlaka ya maji Kibaya KIUWASSA waomba kupandiha bei ya maji

Jumanne Ihucha mratibu wa mamlaka ya maji safi mjini Kibaya, akiomba kuongeza bei ya maji kwa wadau wake, ambapo hatua kadhaa zimefikiwa kama anavyoonekana akiwasilisha ombi lake kwa wadau..
David Ngulla, mwenyekiti wa baraza la ushauri la watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) akiwasilisha hoja kuhusiana na ombi la mamkala ya maji na usafi wa mazingira ya Kibaya kutaka kupandisha bei ya maji..
Mkurugenzi mtendaji wa halm ya Kiteto, Tamimu Kambona, akichangia hoja baada ya kuwasilishwa ombo la mamlaka ya maji Kibaya kutaka kupandisha bei ya maji..
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto (DC) Tumain Magessa akichangia hoja kikao cha wadau wa maji Kibaya..
Ndaki Stephano, (DAS) Katibu Tawala Wilaya ya Kiteto, akichangia hoja kikao cha wadau wa maji Kibaya..
Bodi ya mamlaka ya maji mjini Kibaya wakifuatilia hoja mbalimbali za wadau wa maji Kibaya kuhusu ombi lao la kutaka kupandisha bei ya maji..

Kamati ya ulinzi na usalama Kiteto wakifuatilia mjadala wa maji mjini Kibaya..
 Baadhi ya wananchi wa mji wa Kibaya wakifuatilia kikao cha wadau wa maji..

Bodi ya mamlaka ya maji mjini Kibaya wakifuatilia hoja mbalimbali za wadau wa maji Kibaya kuhusu ombi lao la kutaka kupandisha bei ya maji..


NA. MOAHAMED HAMAD KITETO.

Mamlaka ya maji mjini Kibaya, (KIUWASSA), Wilayani Kiteto mkoani Manyara, imewasilisha mapendekezo ya kutaka kupandisha kwa bei ya maji, ili iweze kujiendesha tofauti na ilivyo sasa kuwa inashindwa kujiendesha

Kwa mujibu wa taarifa katika utaratibu huo ni kwamba, hatua iliyofikiwa ni ya tatu kati ya hatua saba ambazo zinatakiwa kupitiwa ili kuweza kupata baraka za kupandishwa kwa bei ya maji

Akitoa hoja kwa wadau wa maji mjini Kibaya, Jumanne Ihucha, Mkurugenzi wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Kibaya, alisema kwa sasa mamlaka inajiendesha kwa hasara, hivyo ili kuwezesha huduma kupatikana kwa kiwango stahili, kuna kila sababu ya kupandisha gharama za maji

Alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na uzalishaji mdogo wa maji kutokana na kukosekana kwa fedha za kulipia umeme wa kuendeshea mitambo,Kuongezeka kwa mfumko wa bei za bidhaa na vipuri kwaajili ya matengenezo,Uchakavu mkubwa wa mtandao wa usambazaji wa maji mjini Kibaya

Zingine ni baadhi ya wateja kutolipa bili zao za maji kwa muda mrefu, pamoja na vitendea kazi,na uvamizi wa maeneo ya miundombinu ya maji kwa kufanywa shughuli za kibinadamu

Akitoa mapendekezo hayo Bw. Ihucha alisema wanakusudia kuongeza uzalishaji wa maji kwa kujenga miundombinu mipya, wataongeza ukusanyaji wa mapato kama weanavyoshauriwa

Mkurugenzi mtendaji wa hlm ya Kiteto, Tamimu Kambona aliwataka Mamlaka ya maji mjini Kibaya, kuanza kukusanya mapato kwa kutumia mashine ya EFD, na kuwataka kuwa makini baada ya kuachiwa miradi na hlm kama visima walivyochimba vikiwepo vya eneo la ngarenaro na hosp

Kwa upande wa maoni ya baraza la ushauri la watumiaji wa huduma zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) chini ya mwenyekiti wa baraza hilo Devid Ngula, walisema ongezeko la bei linaloombwa na mamlaka ya maji mji wa Kibaya KIUWASA ni kubwa na litasababisha mtikisiko kwa watumiaji

Katika hatua hiyo, mkt huyo alishauri KIUWASSA kupunguza matumizi yasiyo lazima na kuwataka wakusanye madeni yao ambayo hadi sasa yamefikia zaidi ya mil 11.7 badala ya kuwabana wananchi,"Pia katika mapato yao ya zaidi ya mil 11, haionyeshi kama huwa wanakaguliwa jambo ambalo linatia shaka"alisema

Akijibu hoja hizo Ihucha alisema wamepokea mapendekezo yote na kusema kwa sasa kila kituo kuna mita, na wataanza kukaguliwa na mkaguzi kama ilivyopendekezwa.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magessa aliwataka wananchi kulinda miundombinu huku katibu tawala wa Kiteto, Ndaki Stephano akisisitiza mamlaka kuwa makini na kazi weazifanyazo katika kuhudumia wananchi..

Mwisho

Maoni