Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, DC Tumaini Magessa, akifafanua jambo katika kikao cha viongozi wa mila wamasai (malaigwanani)..
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto, DAS Ndaki Stephano, akifafanua jambo..
Mwenyekiti wa halm ya Wilaya ya Kiteto, Lairumbe Mollel Akifafanua jambo,..
Mkuu wa Polisi Kiteto, SP.Fadhili Luoga, katikati akifuatilia kikao cha mila ya jamii ya kifugaji maasai..
Mwenyekiti wa halm ya Kiteto, Lairumbe Mollel, akifafanua jambo..
Na. MOHAMED HAMAD
VIONGOZI wa mila wa jamii ya kifugaji maasai, (Laigwanani) Wilayani Kiteto mkoani Manyara, wameazimia kusimamia mambo matatu, ndani ya jamii yao
Mwenyekiti wa mila wilayani Kiteto Ngayoni Bakari, ameyataja mambo hayo kuwa ni, kutolisha mashamba ya wakulima, kuhakikisha watoto wao wanaenda shule, na kuzuia wizi wa mnyama aina ya punda katika maeneo yao
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto DC Tumaini Magessa, katika kikao hicho alisema, jukumu la ulinzi ni kazi ya jeshi la Polisi akisisitiza kuwa kwa nafasi walionayo viongozi hao wa mila watasaidia kukamata wezi wa punda, pamoja na kufanya Kiteto kuendelea kuwa na amani kwa kukemea mifugo kuharibu mazao ya wakulima
Ndaki Stephano, Katibu Tawala wa Wilaya ay Kiteto, aliwataka jamii ya kifugaji kutambua kuwa Serikali iko kwaajili yao na walivuke ngazi na kujichukulia sheria wanapohitilafiana na wezao jamii ya wakulima
Kwa upande wa Jeshi la Polisi Kiteto, chini ya Mkuu wa Polisi wilaya Fadhili Luoga, aliwataka viongozi hao kuendelea kulipa ushirikiano jeshi la polisi ambalo bila ushirikiano alisema ni ndoto kutokomeza uhalifi..
Jamii ya kifugaji maadai, chini ya viongozi malaigwanani, wameapa kuwa watahakikisha wanakabiliana na mambo hayo matatu ili kufanya Wilaya kuendelea kuwa na amani huku wakishirikiana na jamii zingine
Mwisho.
Maoni
Chapisha Maoni