CCM Kiteto waanza kuchukua hatua kwa wanachama wake

Mhandisi Pashua Sekuwe, katibu wa CCM Wilaya, akifungua kikao cha kamati ya siasa..





CCM Kiteto waanza kuchukua hatua kwa wanachama wake



Na,MOHAMED HAMAD


CHAMA cha mapinduzi CCM Wilayani Kiteto mkoani Manyara, kimeanza
kuchukua hatua za kinidhamu kwa wanachama wake waliodaiwa kukisati
wakati wa Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Sababu zilizotajwa za wanachama hao kuchukuliwa hatua ni kutoonyesha
ushirikiano kwenye uchaguzi huo, ambapo ulidaiwa kuwa na changamoto
zilizotishia CCM kupokonywa nafasi ya kuisimamia Serikali Kiteto.

Kwa mujibu wa kamati ya Siasa ya wilaya, ilielezwa miongoni mwa
mapendekezo ya adhabu hizo ni kufukuzwa uanachana, kutoshiriki
shughuli za chama kwa miezi 33 na kupewa onyo kali.

Akifungua kikao cha kamati ya siasa ya Wilaya,Mhandisi Shekue Pashua,
Katibu wa CCM Wilaya alisema, Chama cha mapinduzi CCM Kiteto, kinaunga
mkono jitihada za Mwenyekiti Rais Dr. John Pombe Magufuli, katika
kukiunda chama upya

"Hatuwezi kuwa kinyumbe na maelekezo ya Mwenyekiti wetu, na hapa
Kiteto, tutafanya hivyo hivyo, ili kulinda maslahi ya chama" alisema
Mhandisi Shekue

Alisema CCM ni chama kinachosimamia Serikali, hivyo hakiwezi kuwa na
watu ambao hawana mchango kukifanya kuendelea kuwa madarakani.

Baada ya mapendekezo hayo, majina yanakusudiwa kuwasilishwa CCM mkoa
wa Manyara kwa hatua zaidi, ambapo taarifa za uhakika zinasema awali
waliyapeleka,majina hayo yaliwasilishwa na kurejeshwa ili kupitiea
upya

Mwisho.

Maoni